JULIO,AMRI SAID WAMPIGA MKWARA MWAMUZI LIGI DARALA LA KWANZA
Posted by
woinde
on
Friday, October 17, 2014
in
MATUKIO
MICHEZO
|
|
Wachezaji
wa timu ya Mwadui FC, wakishangilia goli lililofungwa na Bakari
Kigodeko, katika mchezo wa ligi
daraja la kwanza dhidi ya Panone FC, uliofanyika kwenye Dimba la
Ushirika, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. mchezo huo ulimalizika kwa
sare ya 1-1. |
|
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kwenye dimba la Ushirika, wakifuatilia mchezo kati ya Mwadui na Panone. |
|
Mashabiki
wa Panone wakishangilia goli la kusawazisha lililopatikana katika
dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza, likifungwa na Tony Kigundu. |
|
Shangwe zikaendelea |
|
Kocha
msaidizi wa Klabu ya Mwadui, Amri Said, akizuiwa na mwamuzi wa mezani,
Thomas Mkombozi wakati akijaribu kutaka kumfuata mshika kibendera namba
moja akipinga maamuzi akipinga maamuzi ya kuingia kwa bao la Panone FC
alilodai lilikuwa la utata. |
|
Ubabe ukatumika... |
|
Hapa akimrudisha Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwelo 'Julio' katika eneo lake. |
|
Benchi la Ufundi la Mwadui FC, wa kwanza kushoto ni kocha mkuu Jamhuri Kiwelo 'Julio', kulia. |
|
Julio akitoa maelekezo kwa mchezaji wake |
|
Mwokota mipira akiwa katika pozi. |
|
Sehemu ya Jukwaa kuu likiwa limesheheni mashabiki |
|
Wachezaji wakitoka mapumziko |
|
Mmoja wa viongozi wa Benchi la Ufundi la Mwadui FC, aliamua kuwavaa maaskari wa Jeshi la Polisi. |
|
Balaa la Jamhuri Kiwelo kama kawaida likaendelea.. |
|
Waamuzi wakiondolewa uwanjani kwa Ulinzi mkali muda wa Mapumziko. |
|
Kocha wa Panone FC, Maka Marwisi, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko. |
|
Hivi
karibuni Bodi ya Ligi iliamuru kujengwa Uzio kuzunguka eneo la ndani ya
Uwanja 'Pitch" kwa ajili ya usalama wa wachezaji lakini cha kushngaza
kama inavyoonekana hapo, hizo ni pikipiki "Bodaboda" zikiwa zimeegeshwa
ndani ya uzio huo, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wachezaji hao. |
|
Jamhuri Kiwelo akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. |
|
Heka heka za kuwania mpira ukiendelea katika mchezo huo mkali. |
|
Mchezaji wa Panone FC, akikimbilia mpira |
|
Wachezaji wa Panone FC, wakitoa huduma kwa mchezaji wao aliyeumia. |
|
Hapa wakiwa wamembeba....hili ni tukio la kushangaza na la aibu kweli.. |
|
Benchi la ufundi la Panone FC, walipochukua jukumu ya timu ya usalama ya msalaba mwekundu. |
|
Panone FC, wakifanya mabadiliko |
|
|
Mwadui FC wakifanya mabadiliko. |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia