KILIMANJARO viongozi wa vyama vya Ushirika hapa nchini wametakiwa kuthamini ununuzi wa kahawa iliyo safi na yenye ubora ambao unakubalika katika masoko.
Hayo yamesemwa
hivi karibuni na Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro,
Kasya Kasya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi.
Alisema chama
cha ushirika ni chombo cha kiuchumi, kinapaswa kufanya biashara na kama hawatathamini
bidhaa inayouzwa katika masoko yetu, madhara yake makubwa ni kuendelea kupata hasara.
Amefafanua kuwa
ili kahawa iweze kumwongezea thamani mkulima ni vyema viongozi waliopo katika chama kuhakikisha
wanasimamia kikamilifu, ununuzi wa kahawa ambayo haijachanganywa kitu chochote.
Aidha alitoa
rai kwa wakulima wa zao hilo kuona umuhimu wa kuandaa kahawa yenye ubora ambayo
itawapatia faida kubwa na kuachana na tabia ya kuuuza kahawa mbichi.
Kwa upande
wao wakulima wa kahawa walielezea sababu za kuuza kahawa mbichi, ambapo
walisema kuwa wengi wao wamekuwa wakiuza kahawa mbichi ili kuongeza uzito kwani wanapouza kahawa ambayo imekauka
inapunguza uzito.
Mmoja wa
wakulima hao, Edith Moshi, alisema wakulima wamekuwa wakiwahisha kuuza kahawa
mbichi, ili kuweza kujipatia fedha za kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka
watoto wao shule, huku wangine kwa ajili ya kujitibu.
Kwa upande
wake Meneja mkuu wa KNCU, Honest Temba alisema
kahawa inapokuwa na unyevunyevu, asilimia 13 hadi 19 wanajikuta wanapata hasara
ya mabilioni ya fedha kutokana na ununuzi wa kahawa mbichi.
Temba amewataka
viongozi walioko zamu kwenye vyama vya msingi, kuwa makaini na kazi zao wakati wanaponunua kahawa ili kuwepuka hasara.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia