Wahudumu
wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa wamebeba masanduku ya kura za wajumbe
waliopiga kura za siri kwa Sura ya 11 hadi 19 ya Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa, mjini Dodoma jana. Baadhi
ya wajumbe wa Bunge la Katiba waliopiga kura za hapana wamelazimika
kuondoka Dodoma na kurudi Zanzibar kwa madai ya vitisho walivyopata
kutoka kwa wenzao.Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana jioni
kuwa yeye na wajumbe wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti wa
Bunge, Samuel Sitta kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu
kura hiyo na kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao
wameamua kuondoka Dodoma.Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya
Sitta kuunda Kamati ya Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu
Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na
wajumbe saba zinazoweka njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya
kupitisha Katiba inayopendekezwa.
Wajumbe
waliopiga kura za wazi za hapana kwa ibara zote ni Adil Mohamed Adil,
Dk Alley Soud Nassor, Fatma Mohamed Hassan, Jamila Ameir Saleh, Salma
Hamoud Said, Mwanaidi Othman Twahir na Ali Omary Juma.
Kwa
upande wa Tanzania Bara aliyepiga kura ya hapana kwa rasimu nzima ni
Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), Said Arfi na wajumbe 30 kutoka Zanzibar
wakipiga kura ya siri.
“Baada
ya kupiga kura za hapana leo (jana), walijitokeza wajumbe akiwamo (jina
tunalihifadhi kwa sasa) wakaanza kutuzongazonga,” alisema Salma.
“Walituambia
kuwa tumebaki hadi dakika ya mwisho halafu tunasema hapana kwa rasimu
nzima ili kula fedha za bure, wanasema bora tungeondoka na Ukawa (Umoja
wa Katiba ya Wananchi).”
Hata
hivyo, alipopigiwa simu yake ya mkononi mmoja wa watuhimiwa, alipokea
na baada ya mwandishi kujitambulisha alikata simu na alipopigiwa mara ya
pili alijibu alisema; “Mimi ni mheshimiwa mwana na niko Sudan.”
Salma
alisema miongoni mwa wajumbe hao wakiwamo baadhi ya mawaziri
waliwafuata hadi nje ya ukumbi wakiwatishia kuwa watawafanyia hujuma kwa
kukataa kuunga mkono rasimu hiyo.
“Sisi tumeamua kuondoka kurudi kwetu, hatutaingia tena bungeni maana hivi vitisho vimezidi sasa,” alisema Salma.
Juhudi
za kuwapata wajumbe wenzake kuzungumzia vitisho hivyo hazikuzaa
matunda, lakini Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alikiri kupokea
malalamiko hayo na kwamba amelichukulia kama suala la kisiasa.
Alisema
wajumbe hao hawajasema wametishiwa kufanyiwa kitu gani, bali
walimweleza kuwa wameambiwa kuwa wamekaa pale (bungeni) kwa ajili ya
kupata pesa.
Kuhusu
kukataa kwao kuhudhuria katika Kamati ya Mashauriano, Hamad alisema
hawezi kulitolea jibu kwa kuwa litafanya maridhiano yasifanyike.
Kamati ya Maridhiano
Akitangaza
kuunda kamati hiyo, Sitta alisema ana suala mbele yake ambalo
linahitaji mashauriano chini ya Kanuni ya 54(4) kutokana na baadhi ya
wajumbe kupiga kura ya hapana kwa ibara zote.
Kanuni
hiyo inasema: “Mwenyekiti baada ya kushauriana na kamati ya uongozi
anaweza kuunda kamati ya mashauriano pale linapojitokeza suala
linalohitaji mashauriano.
“Baadhi
ya wajumbe jana (juzi), walipiga kura za hapana kwa ibara zote, jambo
ambalo haliwezekani kuwa hivyo. Kwa kushirikiana na Makamu Mwenyekiti,
nimeunda kamati hii ambayo naomba ikafanye kazi leo,” alisema.
Alisema
kamati hiyo yenye wajumbe tisa itakayoongozwa na Samia na baada ya
kikao chake cha jana itatoa matokeo bungeni. Wajumbe wengine ni Rashid
Mtuta, Shamsi Vuai Nahodha, Omary Yusuf Mzee, Mohamed Aboud, Andrew
Chenge, Dk Asha-Rose Migiro, Dk Francis Michael na Brigedia Jenerali
Hassan Ngwilizi.
“Hawa
watakaa na wale wawili walioniomba kwamba wanataka kusikilizwa kwa nini
wamesema hapana kwa kitendo ambacho inaonekana kama wamepoteza muda
kukaa bungeni ili kukataa Katiba yote,” alisema.
Alitoa
nafasi kwa wajumbe wengine ambao walipiga kura za hapana watakaopenda
kwenda katika kamati hiyo kueleza ni kwa nini waliikataa rasimu hiyo.
Hata
hivyo, kabla ya kuanza kwa upigaji kura jana, Sitta alisema kuwa hali
inakwenda vizuri... “Inshallah hali inakwenda vizuri na dua la kuku
halimpati mwewe.”
Kwa
mujibu wa Kanuni 36(3). Endapo mjumbe baada ya kukataa ibara za Rasimu
ya Katiba, mwenyekiti ataunda kamati ya mashauriano ambayo itasikiliza
hoja zake na kupata mwafaka.
Kanuni
36 (4), baada ya kamati ya mashauriano kukutana na kujadili ibara
inayobishaniwa, itapeleka taarifa ya matokeo ya mashauriano yake kwenye
Bunge Maalumu kwa ajili ya kujadiliwa na ibara hiyo kama ilivyo au baada
ya kuandikwa upya kwa kuzingatia taarifa ya Kamati ya Mashauriano.
Endapo
theluthi mbili haitapatikana kwa mara ya pili, ibara hiyo itahesabiwa
kuwa haikukubaliwa wala kupitishwa na Bunge Maalumu kwa mujibu wa
masharti yaliyowekwa na sheria na kanuni hizi.
TEC yamshukia Sitta
Kauli
ya Sitta kuwa baadhi ya nyaraka kuhusu mchakato wa Katiba Mpya
zinazotolewa na makanisani, “hazina utukufu wa Mungu na ni za kipuuzi”
imepondwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC),
likisema hajui nguvu ya umma.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi
alisema: “Unadhani tulivyotoa waraka tulikuwa tunawataka waumini wafanye
nini? Je, ni kufuata dhehebu lako limesema nini au kufuata kilichomo
katika waraka? Wewe (mwandishi) si Mkristo? Jibu hilo.”
Aliongeza,
“Wenye mapenzi na nchi hii wamfute kichwani Sitta na huo upuuzi
aliosema ni wake mwenyewe. Huyu anadhani kuwa ana akili kuliko mamilioni
ya Watanzania waliopendekeza wanataka kujitawala namna gani?”
Sitta
alitoa kauli hiyo mjini Dodoma juzi wakati akiwatambulisha viongozi 13
kutoka Jumuiya ya Image ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba ya
mjini Dodoma.
Licha
ya Sitta kutotaja taasisi husika, lakini Jukwaa la Wakristo Tanzania
ndilo lililotoa waraka unaotaka kusitishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya
na kusambazwa makanisani.
Waraka
huo ulitolewa kwa pamoja na TEC, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT),
Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (FPCT) na Kanisa la
Waadventista Wasabato (SDA).
“Anadhani
wanaweza kutunga Katiba ya kuwatawala wananchi. Kauli aliyoitoa ni sawa
na kuwapuuza Watanzania na ni sababu ya madaraka tu, maana ndiyo
yanayowapa watu wengi kiburi,” alisema.
Askofu
huyo alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa kauli hiyo ya Sitta maana
yake ni kwamba CCM itabaki milele madarakani na Watanzania hawawezi
kuwafanya jambo lolote.
“Unajua
mtu mwenye kiburi na dharau anayedhani hawezi kuambiwa chochote
unatakiwa kumwacha kama alivyo ila Watanzania ndiyo watakaoamua nini
wanataka katika maisha yao,” alisema.
Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony Lusekelo alisema: “Bunge la Katiba
limemwelemea Sitta na ndiyo maana ameanza kutukana watu.”
Lusekelo
maarufu kama Mzee wa Upako alisema kwa jinsi jamii ilivyogawanyika
katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, ilikuwa jambo la busara kwa
makanisa kutaka kusitishwa kwa mchakato huo mpaka makundi yote
yanayovutana yafikie mwafaka.