Mtalaam
wa Mawasiliano wa Tigo Amani Nkurlu (kulia) akikabidhi tuzo ya ‘Tigo
Best Short Film’ kwa Mtayarishaji wa Filamu kutoka Kenya Mark Maina
katika Maonesho ya Filamu ya Kiafrika Arusha (AAFF) aliyeshinda kupitia
filamu yake mpya iitwayo “Consigned to Oblivion.” Maonesho hayo
yaliyodhaminiwa na Tigo yalifikia tamati juzi.
Mratibu
wa maonesho ya AAFF Nassir Mohamed akionyesha tuzo aliyoipokea kwa
niaba ya Muongozaji filamu kutoka Tanzania Amil Shivji aliyeshinda tuzo
ya ‘Best Short Film’ kwa ukanda wa Afrika Mashariki kupitia filamu yake
mpya iitwayo “Samaki Mchangani.” Akishuhudia kulia ni Mtalaam wa
Mawasiliano wa Tigo Amani Nkurlu.
Wacheza
filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki (Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya,
Tanzania na Zanzibar) wakionesha vyeti vyao ya kuhitimu mafunzo maalum
ya uchezaji na uandaaji wa filamu kutoka wagwiji mbali mbali wa uandaaji
wa filamu barani Afrika.
Wageni
waalikwa mbali mbali na wapenzi wa filamu wakipata burudani kutoka
kundi la Reggae kutoka Tanzania, Kenya na Marekani ‘The Warriors from
the East’ wakitoa burudani.