Akizungumza Dar es Salaam jana kabla ya kuanza kwa
kikao cha siku mbili cha Kamati Kuu ya Chadema (CC), Mbowe alisema Rais
Kikwete si mtu wa kupanga naye ‘dili,’ na kutolea mfano makubaliano
kati ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Rais kuhusu Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
“Tulikutana na Rais Kikwete katika kikao cha TCD
na kukubaliana kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ufanyike Februari
mwakani ili tubadili sheria kwanza na kuboresha daftari la wapigakura.
“Cha ajabu kupitia kwa Waziri Mkuu, Serikali inasema uchaguzi utafanyika Desemba mwaka huu,” alisema Mbowe.
TCD inaundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi
bungeni ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP, huku
vyama visivyo na uwakilishi bungeni vikiwakilishwa na chama cha UPDP
kinachoongozwa na Fahm Dovutwa.
Kwa mujibu wa kanuni zilizotolewa na ofisi ya
Waziri Mkuu ambayo kisheria ndiyo yenye jukumu la kusimamia uchaguzi
huo, fomu ya mgombea uenyekiti wa kitongoji ina sehemu 12 ambazo mgombea
anatakiwa kujaza, ikiwamo nembo ya chama chake cha siasa na nembo ya
halmashauri aliyopo.
Wakati huohuo, wanachama tisa wa Chadema Mkoa wa
Njombe akiwamo Diwani wa Kata ya Njombe Mjini, Aggrey Mtambo wamekamatwa
na polisi kwa mahojiano ya saa nne baada ya kuingia eneo la Kituo cha
Polisi kwa ajili ya kufanya usafi kwa kile walichoeleza kuadhimisha
kumbukumbu ya miaka 15 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Tukio hilo lilitokea saa nne asubuhi jana na
viongozi hao wa Chadema walishikiliwa hadi majira ya saa tisa alasiri
walipowekewa dhamana.
Chadema walifika zilipo ofisi za polisi wilayani
Njombe, kwa lengo la kufanya usafi katika kituo hicho, baada ya kufanya
usafi katika Soko la Wakulima, Soko Kuu na Stendi Kuu ya Mkoa.
Mtambo aliliambia gazeti hili muda mfupi baada ya
kuachiwa kwa dhamana kwamba, walikamatwa na kuwekwa ndani kwa kuwa
walifanya usafi eneo la polisi bila kibali.
“Kwa mujibu wa polisi, wametukamata kwa kuwa
tulienda kufanya usafi bila kibali na gari la taka tuliloenda nalo ni
kama tulitaka kuteka kituo, , ” alisema Mtambo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia