Makundi
ya watu wanaoshangilia, yamempokea Rais Uhuru Kenyatta ambaye amerejea
Kenya baada ya kuhudhuria Mahakama ya Kimataifa ICC, iliyopo The Hague.
Bwana
Kenyatta alihudhuria shauri mahakamani siku ya Jumatano, na kuwa rais wa
kwanza aliyepo madarakani kufika katika mahakama ya ICC.
Rais Kenyatta alipokelewa Nairobi kwa gwaride la heshima na ngoma.
Picha: Bw Kenyatta akiwa na mmoja wa mawakili wake wa utetezi ICC.
Anakanusha
mashtaka dhidi yake ya uhalifu dhidi ya ubinaadam kuhusiana na ghasia
za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zilizosababisha vifo vya watu 1,200
na wengine 600,000 kupoteza makazi.