Uongozi
wa Skylight Band unawaomba radhi mashabiki wake wa Dar es Salaam kwa
kutokuwepo nchini kwa ajili ya kutoa burudani jioni ya leo kwenye uwanja
wao wa nyumbani Thai Village Masaki pamoja na siku ya Jumapili kwenye
Skylight Sunday Bonanza katika kiota cha maraha Escape One kutokana na
kupata mwaliko wa kutumbuiza nchini Oman.
Skylight
Band watarejea nyumbani wiki ijayo na kuendelea na ratiba zao kama
kawaida ambapo siku ya Ijumaa tarehe 10/10/2014 watakuwepo Thai
Village pamoja na Jumapili tarehe 12/10/2014 kwenye Skylight Sunday
Bonanza ndani ya kiota cha maraha Escape One.
Skylight
Band inarudia tena kuwaomba radhi mashabiki wake wa Dar na kuendelea
kuwashukuru kwa sapoti wanayoipata na inawapenda sana.