Ndege za
shirika la ndege la flydubai lililo na makao yake Dubai zilizozindua
safari za kuenda Entebbe na Bujunbura zilitua leo na zilikaribishwa
kitamaduni na saluti za mizinga ya maji na waakilishi rasmi.
Waakilishi wa flydubai (http://www.flydubai.com)
waliongozwa na Hamad Obaidalla, Afisa Mkuu wa Biashara wa flydubai, na
Sudhir Sreedharan, Naibu Mkuu wa Rais wa Biashara wa flydubai (GCC, Bara
Dogo na Afrika), na katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe
walilakiwa na Abraham Byandala, Waziri wa Uganda wa Kazi na
Usafirishaji, na John Okalany, Meneja Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa
Entebbe.
Katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura, waakilishi wa flydubai
walilakiwa na Ciza Virginia, Waziri wa Usafiri, Kazi na Vifaa vya Umma,
na waliburudishwa na wacheza ngoma za kitamaduni.
Kwa
kuzindua safari za ndege za moja kwa moja kila siku hadi Entebbe,
safari mbili za kuunganisha kila wiki za Kigali na safari tatu za
kuunganisha kila wiki za Bujumbura, pamoja na utangazaji wa hivi majuzi
wa njia tatu mpya nchini Tanzania, flydubai imeongeza vituo vyake barani
Afrika mara mbili hadi vituo 12. Zaidi ya hayo, shirika hilo la ndege
linatoa huduma za Kitengo cha Biashara na huduma za mizigo katika kila
moja ya njia hivi mpya.
Akizungumzia
kuhusu uzinduzi wa njia ya Entebbe, CCO wa flydibai Hamad Obaidalla
alisema: "Tunafurahia safari zetu za ndege za Entebbe, moja ya kitovu
kinachoongoza kibiashara barani Afrika. Tukiwa na safari za ndege za
kila siku zinazotoa chaguo la kitengo cha uchumi na biashara,
tutarahisisha utiririkaji wa watalii na biashara kati ya Uganda na Umoja
wa Falme za Kiarabu."
Mjini
Bujumbura Obaidalla alisema: "Tunaamini kwamba bioanuwai tele nchini
Burundi itawavutia watalii kutoka mtandao wetu wote na kwamba zaidi ya
vituo 80 tunavyoendesha vitaipa nchi hii fursa kubwa kuimarisha uhusiano
wake wa biashara."
flydubai
ndio shirika la ndege la kwanza la kitaifa kutoka Umoja wa Falme za
Kiarabu kusafiri Rwanda na Burundi, likisisitiza ahadi yake kufungua
masoko yasiyohudumiwa vya kutosha. Safari yake ya kwanza ya Kigali,
Rwanda ilikuwa mnamo tarehe 27 mwezi Septemba.
flydubai
inatoa safari za kuaminika na za bei nafuu hadi vituo 83 katika nchi
42. Kutoka Entebbe, Bujumbura au Kigali, abiria wanaweza kuweka nafasi
za safari rahisi za kuunganisha kupitia Dubai hadi India, nchi za Ghuba
na vituo mbalimbali nchini Urusi, pamoja na vituo vingine. Kitovu cha
kimkakati cha shirika hilo la ndege kikiwa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dubai, abiria pia wanaweza kunufaika kutokana na
makubaliano kati ya flydubai na mashirika mengine ya ndege, na kuwapa
fursa za safari za kuendelea kwa zaidi ya vituo 200.
Maelezo ya Safari za Ndege:
Entebbe, Uganda
flydubai itaendesha safari saba za ndege kila wiki kati ya Entebbe na Dubai kuanzia tarehe 28 Septemba 2014.
Jumanne,
Ijumaa na Jumapili: FZ622 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Entebbe saa 7:30 usiku saa za ndani, itue katika Kituo cha 2
cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 2:05 asubuhi saa za
ndani.
Jumatatu,
Alhamisi na Jumamosi FZ621 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 10:10 jioni saa za ndani, iwasili
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 8:30 usiku saa za ndani.
Jumanne
na Ijumaa: FZ624 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Entebbe saa 4:10 usiku saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 10:35 asubuhi saa za ndani.
FZ623
imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Dubai saa 6:20 mchana saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa
Entebbe saa 4:40 jioni saa za ndani.
Jumapili:
FZ620 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa
9:15 mchana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dubai saa 3:50 usiku saa za ndani. FZ619 imepangiwa
kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 3:55
asubuhi saa za ndani, iwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Entebbe saa 8:15 mchana saa za ndani.
Jumanne:
FZ620 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa
7:15 mchana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dubai saa 1:50 jioni saa za ndani.
FZ619
imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Dubai saa 1:55 asubuhi saa ndani, iwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Entebbe saa 6:15 mchana saa za ndani.
Nauli za safari ya pande zote
Nauli ya
kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Entebbe hadi Dubai
itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa,
huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola
1,100 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg
uliokaguliwa.
Bujumbura, Burundi kupitia Entebbe
flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Bujumbura na Dubai kupitia Entebbe kuanzia tarehe 30 Septemba 2014.
Jumanne
na Ijumaa: FZ624 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Bujumbura saa 12:55 jioni saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 10:35 asubuhi saa za ndani na
katizo la saa moja mjini Entebbe.
FZ623
imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Dubai saa 6:20 mchana saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Bujumbura saa 11:55 jioni saa za ndani na katizo la saa moja mjini
Entebbe.
Nauli za safari ya pande zote
Nauli ya
kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Bujumbura hadi Dubai
itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa,
huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola
1,100 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg
uliokaguliwa.
Entebbe hadi Bujumbura
flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Entebbe na Bujumbura kuanzia tarehe 30 Septemba 2014.
Jumanne
na Ijumaa: FZ623 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Entebbe saa 11:40 jioni saa za ndani, itue katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Bujumbura saa 11:55 jioni saa za ndani.
FZ624
imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura saa 6:55
jioni saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa
3:10 usiku saa za ndani.
Nauli za safari ya pande zote
Nauli ya
kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Entebbe hadi Bujumbura
itaanzia Dola 400 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa,
huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 900
za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa.
Kigali, Rwanda kupitia Entebbe
flydubai itaendesha safari tatu za ndege kila wiki kati ya Kigali na Dubai kupitia Entebbe kuanzia tarehe 27 Septemba 2014.
Jumatatu,
Alhamisi na Jumamosi: FZ622 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kigali saa 4:30 usiku saa za ndani, itue katika Kituo cha 2
cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 2:05 asubuhi saa za ndani
na katizo la saa moja mjini Entebbe.
FZ621
imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Dubai saa 10:10 jioni saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kigali saa 3:30 usiku saa za ndani na katizo la saa moja mjini
Entebbe.
Nauli za safari ya pande zote
Nauli ya
kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Kigali hadi Dubai itaanzia
Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli
ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 899 za
Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa.
Tiketi za safari hizo za ndege zinaweza kununuliwa kuanzia leo kutoka tovuti ya flydubai (flydubai.com),
Kituo chake cha Simu (+971) 600 54 44 45, maduka ya usafiri ya flydubai
au kupitia wabia wa usafiri. Taarifa na maelezo zaidi ya huduma za
shirika hili za ukodishaji gari na bima ya safiri pia zinaweza
kupatikana kwenye flydubai.com.