Marehemu Yesaya Ambikile Mwakalekamo
'YP' amezikwa hii leo katika makaburi ya Changombe jijini Dar es salaam.
Marehemu YP alifariki jana baada ya kuugua kifua na kulazwa katika Hospitali ya Temeke hadi mauti yalipo mkuta.
Awali
kabla ya maziko hayo YP aliagwa na ndugu jamaa na marafiki zake katuika
viwanja vya sigara Chang'ombe ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa
Bongo fleva na Bongo muvi walihudhuria.
YP
kabla ya kuhamia katika sanaa ya uimbaji na kuibuka na kundi la wanaume
Family alikuwa akifanya sanaa ya maigizo na vichekesho akiwa kundi moja
na wasanii, Masanja Mkandamizaji, Mpigapicha maarufu na Blogger Mroki
Mroki, Kiwewe, Dokii enzi hizo wakiwa na kundi la Get Well Generation
lililokuwa chini ya Dokii na kurusha michezo yake Star Tv.
YP enzi za uhai wake aklitamba na nyimbo kama 'Ulipenda
Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama
'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi'
na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family pia alivuma na wimbo wa Binadamu Visa alioimba na swahiba wake,
Y-Dash.
Kiongozi wa kundi la Yamoto Band na TMK, Mkubwa na Wanawe, Saidi Fela akizungumza wakati wa msiba huo.
Juma Nature kutoka TMK Wanaume Halisi akizungumza.
Mh Temba nae akizungumza...
Mmoja wa waigizaji aliyehudhuria mazishi hayo, Jacob Steven 'JB' akizungumza.
Ilikuwa ni vilio kutoka kwa kila mtu aliyehudhuria mazishi hayo.