Halmashauri ya Jiji la Arusha hii leo chini ya uongozi wa Meya
wake Gaudensi Lyimo imezindua kampeni endelevu ya kuweka Jiji na mitaa
yake katika mazingira safi.
Uzinduzi huu unafuatia tukio la Jiji hilo kuibuka kinara wa usafi kwa majiji yote Tanzania takribani wiki moja iliyopita.
Aidha Halmashauri hiyo imetoa zawaki kwa Kata zake zilizofanya vizuri
kwa usafi zikiongozwa na Kata ya Themi na Sekei. Diwani wa Kata ya
Themi ni Mh Menace Kinabo.