TASWIRA YA RIPOTI YA HALI YA BIASHARA YA MAZAO YATOKANAYO NA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA YAZINDULIWA DAR



Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kushoto), akionesha Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo, Dk.Fidelis Myaka.


Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Raphael Daluti Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Mhandisi Raphael Daluti (katikati), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo.


Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo, Dk.Fidelis Myaka (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.


Mtafiti Mkuu wa Kilimo wa Costech, Dk. Emmarold Mneney (kulia), akitoa mada fupi kuhusu maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji wa Sekta mbalimbali hususan ya kilimo.


Kaimu Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech), Dk.Nicholas Nyange (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.


Wadau wa sekta ya kilimo wakiwa kwenye uzinduzi huo.


Wanahabri wakichukua taarifa hiyo.


Wadau wa sekta ya kilimo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.


Waziri Zambi na viongozi wengine wakiwa meza kuu.


Uzinduzi ukiendelea.





Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.


NAIBU Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amesema Tanzania haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji wa Sekta mbalimbali hususan ya kilimo.

Kauli hiyo aliisema wakati akizindua Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi.

"Jukumu letu ni kushirikiana na wadau wote kuhakikisha tunakuwa na matumizi salama na endelevu ya bioteknolojia ili kuiondolea wasiwasi jamii kuhusu dhana iliyopo ya athari zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa" alisema Zambi.

Alisema kutokana na mantiki hiyo, Serikali imeweka mikakati mbalimbali katika kushughulikia masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya mwaka 2010 yenye lengo la kujenga uwezo wa kutumia teknolojia hiyo kwa kuzingatia faida zilizojidhihirisha katika kuboresha afya ya wanyama na binadamu, kilimo, viwanda na mazingira.

Zambi alisema sera ya taifa ya kilimo ya mwaka 2013 inatamka kwamba uelewa mdogo wa umma kuhusu matumizi ya bioteknolojia unachangia kuwepo kwa upokeaji mdogo wa teknolojia hiyo kwa madhumuni ya kuongeza matumizi ya mbinu za bioteknolojia ya kilimo katika uzalishaji, tija na kipato kwenye sekta ya kilimo.

Kaimu Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech), Dk.Nicholas Nyange alisema teknolojia hiyo mpya ya uzalishaji wa mazao ni muhimu sana hapa nchini katika sekta ya kilimo.

Mtafiti Mkuu wa Kilimo wa Costech, Dk.Emmarold Mneney alisema changamoto kubwa waliyonayo watafiti hapa nchini ni pesa na kuwa wanahitajika kutoka katika utafiti wa ndani na kutoka nje kama wafanyavyo wenzao wa nchi za Uganda, Kenya ambao tafiti zao zimefanikiwa katika kilimo cha mahindi, pamba na mohogo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post