Hatimaye mwanamuziki nchini Tanzania,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’, apumua baada ya kuwa na mawazo kutokana na
sakata la kusambaa kwa picha zake chafu ambazo zilipigwa alipokuwa
akitumbiza nchini ubelgiji mwezi uliopita.
Akihojiwa na runinga moja nchini amesema
kuwa alikuwa na hofu sana na alikuwa hapati usingizi kutokana na jambo
hilo kufika hadi Bungeni, jambo ambalo Serikali iliamua BASATA kumfanyia
mahojiano.
Amesema kuwa anamshukuru Mungu leo
alienda BASATA, kuitika wito aliotumiwa juzi wameongea na anashukuru
wamemuelewa na kudai kuwa hakuna tena tatizo kwani wale ni kama wazazi
ambao kazi yao ni kuwaonya mtoto.
Ameongeza kuwa aliwaeleza tukio zima
lilivyotokea na kumuelewesha kuwa mwangalifu katika mavazi kitu ambacho
amedai ni sahihi kabisa na amewashukuru kwa sababu wamemuelewa na kudai
kuwa sasa ana furaha na amani tele.