BREAKING NEWS

Tuesday, June 16, 2015

MAFUNZO YA MAAFISA WA NGAZI YA JUU YA JESHI LA WANANACHI YAAHAMISHWA

 
SERIKALI imehamisha rasmi mafunzo ya maafisa wa ngazi za juu wa jeshi
la wananchi wa Tanzania,kutoka chuo cha maafisa wa awali cha TMA,
kilichopo Monduli na kuyapeleka Duluti, Tengeru wilayani Arumeru.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa,
Dakta Hussein Mwinyi, alipokuwa akitunuku vyeti kwa maafisa wa ngazi
za juu majeshini wapatao 38 wa kozi ya Unadhimu kutoka Tanzania na
mataifa rafiki.

Waziri, Mwinyi, amesema kuwa mafunzo ya maafisa wa ngazi za juu wa
jeshi kuanzia Julai mwaka huu yatafanyika kwenye chuo kipya cha
Duluti,wilayani Arumeru.

Kozi ya ukamanda na unadhimu kwa maafisa wa ngazi za juu jeshini
ilikuwa ikifanyika kwenye chuo cha maafisa wa ngazi ya awali wa jeshi
cha TMA.

‘’leo ninahitimisha rasmi mafunzo ya maafisa wa ngazi za juu jeshini
kwenye chuo hiki cha TMA,na mafunzo yatakayoanza Julai mwaka huu
yatafanyika kwenye chuo kipya cha maafisa wa ngazi za juu jeshini, cha
Duluti, wilayani Arumeru,”alisema waziri.

Amesema mafunzo hayo namba 29 ya 2014/15 mbali na uongozi na unadhimu
pia yamehusisha kozi ya Uhasibu ngazi ya Diploma na Diploma ya juu
waliyoipata kutoka chuo cha Uhasibu cha Arusha, ambacho ni cha
serikali.

Elimu hiyo ya uhasibu itawasaidia kuboresha utendaji wao na
kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kiusalama,kiuchumi na
kijamii .

Mafunzo hayo  ya uongozi na unadhimu jeshini  yameshirikisha maafisa
27 wa ngazi za juu jeshini la wananchi, JWTZ,na maafisa 11wa ngazi za
juu kutoka majeshi  ya nchi rafiki  yametumia wiki 48 na yanasaidia
kuimarisha mahusiano na nchi za ukanda wa afrika.

Nchi hizo ni Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Namibia,Rwanda na  Burundi.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanawawezesha  kupata msingi  wa kutoa
maamuzi kwa wakati  sahihi  na kufanya kazi kwa viwango vya hali ya
juu vya kimataifa.
Awali mkuu wa chuo cha TMA,Meja general  Ezakiel Kyunga, amesema kuwa
wahitimu hao  walisoma kozi mbili moja ya kijeshi na nyingine ya
kiraia ambayo ilihusu uhasibu  .

Amesema kukamilika kwa chuo cha maafisa wa ngazi za juu jeshini ,ambao
ni kuanzia cheo cha meja na kuendelea kutawezesha  kuendesha mafunzo
kwenye eneo ambalo linatosheleza mahitaji .

Kyunga,amesema ndani ya chuo hicho cha TMA,kulikuwa na vyuo
viwili,ambapo chuo cha maafisa wa ngazi za juu walikuwa wameazimwa
miundo mbinu na maeneo ya chuo sasa chuo hicho cha TMA, na
kitaendelea kutoa mafunzo kwa maafisa wa awali.

Akielezea mafunzo hayo, Meja Fred Muchera,kutoka Kenya, amepongeza
mafunzo hayo na kueleza kuwa wamenufaika sana na kozi hiyo ,pia
amepongeza ukarimu wa watanzania na kusema kuwa unajenga urafiki na
udugu

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates