MKUTANO WA TANO WA WADAU WA NSSF WAMALIZIKA LEO JIJINI ARUSHA


 Mtaalam wa maswala ya Saikolojia, Chris Mauki akiwasilisha mada iliyohusu maswala ya Saikolojia, wakati wa Mkutano wa tano wa Wadau Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliomalizika leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza leo wakati wa kumalizika kwa Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
MC wa Mkutano huo, Bi. Sauda Simba akisema chochote.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Felix Ntibenda ili aweze kutoa hotuba ya kufunga Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha leo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Felix Ntibenda akitoa Hotuba yake wakati wa kufunga Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha leo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Mh. Christopher Kangoye akifatilia mkutano huo.






Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post