Makongoro Nyerere
MBUNGE wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere leo amerejesha fomu ya
kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM, baada
ya kukamilisha zoezi la kutafuta wadhamini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CCM White House,
amesema CCM isipokuwa makini katika uchaguzi wa mwaka 2015, chama
kitaporwa na vibaka, wezi na mafisadi.
Amesema, mafisadi, wezi na vibaka wanajulikana hivyo wanachotakiwa ni kuwa makini kwani wakiporwa hawatakipata tena.
Makongoro amesema, waasisi waliwaasa wasikubali kutawaliwa tena lakini
tunapoelekea chama kikiporwa watakuwa wameruhusu kutawaliwa tena.
Amesema, CCM sio ya wezi, mafisadi na vibaka bali ni uridhi wa watanzania walio wengi.
Kada huyo imekiri kupata ushirikiano wa kutosha katika mikoa yote 30 aliyopita na kufanya kazi yake kuwa rahisi.
Amesema kuwa maelekezo ya chama ameyamaliza anachosubiri ni maamuzi ya chama, pia amekiomba chama kitende haki katika kutuchuja.