KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman
Kinana akipokelewa na kamati ya Ulinzi na Usalama usiku huu ndani ya wilaya
Kahama mkoani Shinyanga tayari kwa mapumziko,ambapo kesho ataianza rasmi
ziara yake katika kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani
Kagera,Ndugu Kinana ndani ya Biharamulo atapokea taarifa za chama na
Serikali na baadae kuzungumza na Wafugaji wa kanda ya Ziwa (Mikoa ya
Geita,Kagera,Mwana na Shinyanga) na baadae kueleke Bukoba
mjini.
Ndugu Kinana amewasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera
kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010
na kuimarisha uhai wa chama,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
akipokelewa na Mbunge wa jimbo la Nzega usiku huu Dkt.Hamis
Kingwangalla,mara baada ya kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera
kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa
chama.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
akipokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho usiku huu wilayani Nzega
mkoani Tabora akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya
kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010
na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
akiwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali mara baada ya kuwasili
wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya
kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010
na kuimarisha chama.Ndugu Kinana pia aliwashukuru wakazi wa wilaya hiyo kwa
kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kujenga chama na
nchi kwa ujumla
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
akiwashukuru wapenzi na washabiki wa chama hicho wilayani Nzega usiku huu kwa kumpokea
vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kukijenga na kukiimarisha
chama na nchi kwa ujumla
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
akimshukuru Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla kwa mapokezi mazuri
wilayani humo,ndugu Kinana amewasili wilayani humo mnamo majira saa nne
usiku na ushehe akitokea jijini Dar kwa basi maalum akiwa emeambatana na
ujumbe wake akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi
Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla akitoa ufafanuzi
wa jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman
Kinana .
PICHA NA MICHUZI JR.KAHAMA.