Picha na maktaba
Na Woinde Shizza,Arusha
Mamlaka
ya Chakula na dawa(TFDA) na Shirika la Viwango nchini(TBS), wameshauriwa
kuwadhibiti zaidi wafanyabiashara wasio waaminini ambao wanaingia nchini bidhaa
sizizo na ubora kwani wanaporomosha uchumi.
Meneja
masoko wa kampuni ya Wrigleys (EA)
Company Ltd, Emanuel Laswai, alitoa kauli hiyo juzi, katika uzinduzi wa bidhaa
mpya za kampuni hiyo ya Doublemint
nchini Tanzania.
Laswai
alisema, uingizwaji wa bidhaa feki na zisizo na ubora zina athari za kiuchumi na kiafya kwa watumiaji wa
bidhaa hizo.
“sisi
kampuni yetu kwa mwaka tunalipa kodi Tsh 120 milioni, lakini inaumiza kuona
kuna bidhaa zinaingizwa nchini kinyamela bila kulipiwa kodi”alisema
Alisema
bidhaa zao zote kabla ya kuingia sokono lazima ziidhinishwe na vyombo vya
ukaguzi wa serikali kama TBS na TFDA.
Mkaguzi
wa vyakula, dawa, vipodozi ,wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA,kanda ya
kaskazini, Barnabas Jacob, akizungumzia tatizo la uingizwaji bidhaa feki
alisema Mamlaka hiyo, imeendelea kudhibiti na kukamata na kutekeleza bidhaa
hizo.
Jakob
alisema milango ya TFDA, iko wazi kwa kila mwananchi
kutoa taarifa ya kuwepo kwa bidhaa hatarishi katika mazingira yeyote ili ziweze
kuchukuliwa hatua za kudhibiti bidhaa
zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.
Kwa
Upande wake, Afisa uhusiano wa shirika
la viwango nchini(TBS) Roida Andusamile akizungumza na Mwananchi alisema TBS
itaendelea kudhibiti bidhaa zisizo na ubora kuingia nchini kwa kuanza kudhibiti bidhaa hizo kutoka nchi
zinapotoka.
Hata
hivyo, alisema ni wajibu wa wananchi pia kutoa taarifa TBS wanapobaini bidhaa
zisizo na ubora katika soko au ambazo bado hazijaidhinishwa na vyombo vya
serikali, ili kuweza kuchukuliwa hatua mara moja ya kuwadhibiti na kuwakamata
wahusika.