HII NDIO TASWIRA YA MOTO ULIVYOWAKA NDANI YA LINDI WAKATI MHESHIMIWA BERNARD MEMBE AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS 2015

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwapungia mkono umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa, wakati alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe wakati akiwahitubia wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa, wakati alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.
Ujumbe mwanana kutoka kwa wananchi wa Lindi.
Wakazi wa Lindi wakimsikiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe wakati akiwahitubia wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa, wakati alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.
Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto waliokaa), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana. Wengeni (kutoka kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Adelina Gefi na Mke wa Waziri Membe, mama Dorcas Membe.
Wananchi wakifuatilia matangazo yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja.
Msanii Peter Msechu akiimba mara baada ya kumaliza kutangaza nia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post