WAZAZI TUMIENI MDA MWINGI KUKUAA NA WATOTO WENU NA SIO KUWAACHIA WAFANYAKAZI


 Afisa ustawi wa jamii  jiji la Arusha Saumu kweka akiwa anaongea  katika mkutano huo

Na Woinde Shizza,Arusha

Wito umetolewa kwa wazazi kutumia mda mwingi kukaa na watoto wao ili

kuwaepusha na vishawishi mbalimbali ambavyo wanaweza kuvipata.



Hayo yamebainishwa na  Afisa ustawi wa jamii wa jiji la Arusha Saumu
kweka wakati akiongea na wazazi ,walimu  na wanafunzi juu ya adhari
zinazoweza kumapata mtoto wakati kipiondi ambacho autaweza kuwa nae.



Alisema kuwa kumtelekeza mtoto kunaweza kusababishia vitu vingi
vikiwemo mimba za utotoni kwa upande wa watoto wa kiume kulawitiwa
pamoja na kujifunza tabia chafu ambazo zinamuharibu mtoto huyo.



Alisema kuwa kumekuwa nawazazi wengi wamekuwa  wanafanya wafanyakazi wa
ndani kama walezi hali ambayo inapelekea watoto kujifunza tabia chafu
kwani wasichana wengi wamekuwa hawawafatilii watoto vizuri kama jinsi
mzazi ungekuwa unamfatilia.



“unakuta kipindi hichi wazazi wengi wanajidai wapo bize kutafuta hela
hawezi ata kumuangalia mtoto  hawezi kufatilia mwenendo ya mtoto kitu
ambacho mtoto inafikia mahali anafanya kitu anachokitaka  na hii
inapelekea kwa mfano mtoto wa kike umemuacha umfatiliii wewe uko
kazini umemuacha na mfanyakazi w akiume anaweza kumfanya chochote au
pia mtoto unamuacha anazurura anaweza kukutana na wababa huko
akawadanganya na vichipsi mayai akaenda na mtoto sababu ukai na mtoto
ukampa maitaji anayoyataka sasa akienda kupew achipsi uko utajua
mwishowe ndio unaletea mimba nyumbani saa nyingine watoto wa kiume
ndio wanakuw amashoga”alisema saumu.



Aidha aliwataka wazazi ambao ni wakali kupunguza ukali kwa watoto wao
ili iwapo mtoto atafanyiwa kitu chochote au atakubwa na kitu chochote
iwe rahisi kumuelezea mzazi kwani kuna wazazi wengine wanakuwa wakali
mpaka watoto wanashindwa kuwaeleza matatizo ambayo wanayo.



Kwa upande mwalimu mmoja wapo aliyejitambulisha kwa jina la Gwantu
Mwakabungu aliwaomba wazazi wenyehela kupunguza kuwapa fedha nyingi
watoto wao kwani kitendo cha kuwapa fedha nyingi watoto wao
kinawapelekea waatoto kuwa na zarau hata kwa walimu wao kutokana na
fedha walizo nazo.
Aidha aliiomba serekali kuunda sheria ambayo itazuia wanafunzi kuwa na
simu mashuleni na hata manyumbani kwani kwa kufanya hivyo itasaidia
kupunguza mmonyoko wa maadili kwani simu nyingi zimekuwa zikiwapotosha
wanafunzi wengi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post