WANAJESHI WATAKIWA KUTOKUVUNJA SHERIA YA NCHI



Wanajeshi nchini wametakiwa kutokuwa tayari kutumika kinyume na taratibu za  kijeshi na  maadili ya kazi yao ili kuweza kuepuka uvunjifu wa amani iliyoko na kuweza kutunza nidhamu ya jeshi iliyoko nchini.

Aidha  ameeleza kuwa endapo wanajeshi watakubali kufanya vitendo kinyume na maadili yao wanaweza kusababisha hali ya hatari nchini na kupoteza imani na jeshi la nchini.
 
Hayo yameelezwa na Mkuu wa utumishi na wa jeshi la wananchi wa Tanzania  Meja Generali  Mritaba Venanti wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa askari wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania yaliyofanyika katika kambi ya kijeshi ya jkt oljoro iliyopo  kata ya Terati  katika wilaya ya Halamashauri ya jiji la Arusha katika Mkoa wa Arusha.
 
Aliongeza kuwa na kuwataka askari wake kuacha kujichukulia sheria mkononi na kufanya vitendo ambavyo viko kinyume na kanuni na taratibu za kijeshi na hata katiba ya nchi ili kuweza kuwa askari wa mfano wa kuigwa na kuweza kuendana na nidhamu waliyopewa wakiwa katika mafunzo yao ya uaskari jeshini.

Na endapo askari yeyote atangundulika akivunja maadili ya nchi sheria zitachukua mkondo dhidi yake ili  kuweza kurudisha nidhamu jeshini na kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na mipaka ya Tanzania na kuweza kudumisha amani iliyopo nchini.

‘’nawasihi nyie maaskari tunzeni nidhamu ya jeshi jiepushe na mambo ya vurugu,uvunjifu wa amani na endapo kuna atakayebainika anakwenda kinyume atachukuliwa hatua kali za kijeshi bila kuona huruma ‘’alisema  Mritaba

Pia aliongeza kuwa wanapaswa kutunza afya zao ili kuepuka kupata maambukizi ya ukimwi  ambayo yanaweza  kupunguza a nguvu kazi ya Taifa ili kuwa na kizazi  ambacho hakina maambukizi na kuongeza ufanisi katika kazi zao.

‘’Hivi sasa kumekuwepo na baadhi ya watu wamekuwa hawako makini na afya zao hali inayopelekea kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kupunguza ufanisi wa kazi zao na hasa utelekezaji  wa kujenga taifa na usalama wa raia wao’’ alisema Mritaba

Kwa upande wake Mkuu wa mafunzo ya awali ya Kijeshi Kihangaiko iliyopo  Kibaha Jijini Dar es salaam, Luten Kanali  Ramadhani Churi  alisema kuwa mafunzo haya ni kundi la 33 ya askari wapya kwa kikosi cha 883 jk ambayo yataleta tija na ufanisi katika jeshi la wananchi wa Tanzania  ambayo wamepewa mafunzo ya vita na mbinu mbalimbali katika kupambana kwenye kazi za kijeshi.

Alisema katika kipindi hicho wameonyesha nidhamu ya hali ya juu huku kila mmoja akitambua wajibu wake uliomleta katika kambi  mbali na changamoto za baadhi yao kutoroka mafunzo.
 
Hata hivyo mbali na kufanikisha kwa kumalizika kwa mafunzo hayo bado kumekuwepo na changamoto ya utawala na mafunzo kutokana na mazingira mapya ya mafunzo hayo .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post