MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu
Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kusema hawezi kumrudia aliyekuwa
mpenzi wake, msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Salma Jabu ‘Nisha’.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, Nisha alisema
amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa ana
mpango wa kurudiana naye, jambo
alilosema haliwezekani kwani kwake hana
tabia ya kula matapishi.
“Siwezi kurudiana na Nay, kwanza ana mwanamke mwingine na kuzaa naye
japo wameachana, mwanzo nilimuogopa sana nikimuona, lakini hivi sasa
nimeshamzoea, tumebaki kama kaka na dada, suala la mapenzi haliwezi
kujirudia tena,” alisema.