JOSHUA NASSAR ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI.
Posted by
woinde
on
Thursday, June 04, 2015
in
Habari
MATUKIO
|
|
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar aiwa amepanda kwenye Lori
lililokuwalikibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji
kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe
katika jimbo hilo. |
|
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi
katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa
ajili ya umwagiliaji. |
|
Mbunge
Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo
hilo. |
|
Mbunge
Joshua Nassar akizungumza na mmoja a wanakiji cha Karangai huku akiwa
amembea mtoto muda mfupi baada ya kumaliza hatua za awali za uwekaji
wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya
umwagiliaji. |
|
Mbunge
Joshua Nassar akizungumza na baadhi ya kina mama ambao mingoni mwao
wanajishughulisha na shughuli za kilimo alipotembelea kijiji cha
Karangai kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa chanzo cha maji kwa
ajili ya umagiliaji katika kijiji hicho.
Na Dixon Busagaga
wa Globu ya jamii kilimanjaro
MBUNGE wa
jimbo la Arumeru Mashariki
Joshua Nassar jana ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai
kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo
kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Zoezi hilo
lilo anza majira ya saa 3
asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassar
akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto
kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.
Akizungumza
katika eneo hilo ,Nassar
alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa
baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya
kutoshja.
“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa
siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili
ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia
lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna
anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika
ugali na kazi ikaendelea”alisema
Nassar.
Nassar
aliwashukuru ijana zaidi ya 300
pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia
moyo.
|
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia