Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, Ismail Juma akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma
zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo
mtu yeyote anaweza kujionga alipokuwa akiongea na madereva wa taxi wa wilaya Ilala jijini Dar
Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi,
Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akizungumza na madereva wa taxi wa wilaya ya Ilala(Hawapo pichani) kuhusu kutii sheria za barabarani na kuwasisitiza kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa azungumza jambo na madereva wa taxi wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akijibu maswali ya baadhi ya madereva
Madereva wa Taxi wa wilaya ya Ilala wakiuliza maswali kwa Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa mkutano wao
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akiwaelekeza madereva wa Taxi jinsi yakujiunga na mfuko huo
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akimpa
maelezo mmoja wa madereva wa Taxi wilaya ya Ilala aliyeamua kujiunga na mfuko
wa Peisheni wa PSPF
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akimtolea ufafanuzi kuhusu faida za mfuko wa PSPF wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka(kushoto) akimuonesha mmoja wa madereva ili aweke alama ya dole gumba kwenye fomu za Uchangiaji wa Hiari
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akielezea jinsi ya
ujazaji fomu za Uchangiaji wa Hiari kwa baadhi ya madereva waliovutiwa kujiunga
na mfuko wa Peisheni wa PSPF
Na Mwandishi Wetu
Madereva
taxi katika wilaya ya Ilala jijini dar es salaam wapokea elimu kutoka
kwa mfuko wa pensheni wa PSPF na kuweza kujiunga na mfuko huo ili
kuhakikisha wanawekeza katika mfuko huo kwa manufaa yao hapo baadae
kutokana na kazi zao wanazozifanya kila siku za udereva kuwa ni kazi za
kawaida na kuona kuwa Pspf ndio kimbilio kwa madereva hao
Akizungumza wakati wa mkutano huo Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva Tax ili kuweza
kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao mbalimbali
yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko huo wataona
matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na
familia hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao
ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la
nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia
Mkuu
wa kitengo cha elimu wa jeshi la polisi,kikosi cha usalama barabarani
makao makuu , Abel Swai wakati akitoa elimu ya usalama barabarani
amewaasa madereva wote nchini hususani kwa madereva walio weza kufika
katika mkutano huo wa madereva tax kuweza kuwekeza katika mifuko ya
jamii ni jambo muhimu hasa ukizingatia kwa hali ya sasa maisha kuwa ya
kawaida na uchumi wanchi yetu kuporomoka amewaomba madereva kutumia
fursa zinazo tolewa na mfuko wa pensheni wa PSPF ili wawe na akiba ya
mafao yao pindi kazi zinapo isha na hata kuweza kufaidika na mambo
mbalimbali katika mfuko huo
Pia
mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat
Sylvery Tirumanywa amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani
maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo
,hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa
umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu
iajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo
barabarani,aliongeza kuwapa shukrani mfuko wa pensheni wa Pspf kwa hatua
ya kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili
kuhakikisha mabadiliko ya wananhi mbalimbali yanatokea kimaisha
,elimu,afya na mengine mengi.
Miongoni
mwa madereva waliohudhuria katika mkutano huo wameupongeza mfuko wa
pesheni wa PSPF kwa kuweza kuwajali kwa kuwapa elimu juu ya mfuko huo
pia wameahidi kushiriki vilivyo katika kujiunga na mfuko huo ili
kuhakikisha maisha yao yanaenda sambamba na hadhi ya jina na ubora wa
kazi zinazofanywa na PSPF,
”kwani
tumeiona fursa kutoka PSPF hivyo hatuna budi kujiunga na mfuko huu
kwani fursa ni kuthubutu,kuhiari, kutendana kuamua na uamuzi tulio
uchukua ni kujiunga na PSPF kwa manufaa ya kwetu pia ya taifa kwa ujumla
“pia wawasisitiza kuendelea kueneza elimu katika mkoa wa dar es salaam
wote na hata nje ya mkoa ili watu watambue fursa zinazo tolewa na PSPF.