Mzee wa heshima akielezea historia ya umiliki wa ardhi miaka ya nyuma ukilinganisha na sasa.
Wanakijiji wakifuatilia tukio la makabidhiano ya hati za hakimiliki za kimila za vijiji vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vilivyopo wilayani Hanang’.
Makko
Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na
changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa
kupima mipaka katika vijiji husika
Baadhi ya akina mama wa Kijiji hicho wakifuatilia tukio
Eveline Mirai, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' alitoa
wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu
mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa
wameikubali.
Laurent
Wambura Meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam aliwapongeza wakazi
wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao walipokea
hati zao siku hiyo.
Mkutano ukiwa unaendelea huku wanakijiji wakifuatilia
Mmoja wa wanakijiji akiongea wakati wa Shughuli hiyo ya kukabidhi hati
Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel akizungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mreru James Gejaru akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chake.
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Dirma Agustino Majawa akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chake
hati ya hatimiliki ya kimila
Mwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yake
Mwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yake
Wananchi na viongozi wa Serikali ya kijiji wakipitia kwa makini hati za hakimiliki za kimila za ardhi.
Sherehe zilipambwa na ngoma ya wa-Barbaig
Na mwandishi wetu
Wenyekiti
wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za
kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa
mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwa ufadhili uliotolewa na shirika la
Oxfam kupitia shirika la Ujamaa Community Resource Team - UCRT.
Vijiji hivyo vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vimekabidhiwa hati hizo na katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John
Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika hafla fupi
iliyofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya
100 kutoka katika vijiji hivyo vinne.
Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji hivyo vinne, Mbisha
Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi aliyashukuru
mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi
na kuwasaidia kupata hati za hakimiliki za ardhi ya vijiji. "Sisi
kama wafugaji tulikua hatujui thamani ya ardhi yetu, sasa tumeamka na
kujua haki zetu na manufaa ya kuwa na cheti cha umiliki wa ardhi",
aliongezea.
Aidha
mwenyekiti huyo alisema vijiji vyao kupata hati za hakimiliki za ardhi
itawasaidia kuwa na eneo la pamoja la malisho na itawasaidia kuwa na
nguvu zaidi ya kuilinda ardhi yao na kuisimamia vyema hali ambayo
itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi.
Katika hatua nyingine, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' Bi Eveline Mirai aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwasaidia wakina
mama wajane nao kupata hati za hakimiliki za maeneo yao iliyoenda
sambamba na kusaidia vijiji hivyo vinne kupata hati za vijiji.
Eveline
alitoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa
sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa
wameikubali. “Mtakapoheshimu mipaka, hatutakua na migogoro ya ardhi” na
akawataka wananchi wenye maeneo yao kuhakikisha wanapata hati za
hakimiliki za maeneo yao ili wayamiliki kisheria.
Naye
meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam Laurent Wambura aliwapongeza
wakazi wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao
walipokea hati zao siku hiyo. "Ukilinda
maeneo ya wafugaji maana yake ni kwamba umewahakikishia maisha yao,
tunapenda kuona haki za wafugaji zinapatikana" aliongezea.
Wambura
aliishukuru serikali hususani Halmashauri ya wilaya ya Hanang’ kwa
ushirikiano mkubwa ambao wameutoa kufanikisha zoezi hili na akatumia
fursa hiyo kutoa wito kwa serikali kushirikisha mashirika na wadau
mbalimbali wa maendeleo wakati wa ugawaji wa maeneo ya ardhi za vijiji
kwani wanapogawa vijiji wakati mchakato wa upimaji unaendelea ni hasara
kwa mashirika hayo kwani aidha yanalazimika kuanza kazi upya au
kushindwa kwa sababu tayari fedha zinakuwa zimetumika na tatizo kwa
wananchi linakuwa halijatatuliwa.
Naye Makko
Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na
changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa
kupima mipaka katika vijiji husika.
Changamoto
nyingine ni pamoja na udhaifu katika uongozi wa serikali ya vijiji
ambazo huchelewesha mipango lakini pia kuchelewa kupata ripoti ya
matumizi ya ardhi kutoka wizarani nayo ni changamoto.
Naye Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John
Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo, alipozungumza kabla ya
kukabidhi rasmi vyeti hivyo alizitaja faida za kumiliki ardhi kisheria
kuwa ni pamoja na ardhi
ile huwezi kupokonywa na mtu kirahisi, utajua mipaka ya eneo lako
ambayo huwezi kuingiliwa na mtu na vilevile inaweza kuwa rasilimali
baadaye ukapata fedha kukuwezesha kufanya vitu vingine zaidi.
Akitolea
mfano, John alisema "Mara nyingi wakina mama huwa wanakosa haki yao
pale mume anapofariki, huwa ananyanganywa mali yote ikiwa ni pamoja na
ardhi wakati anaachiwa watoto awatunze, lakini wanapokuwa na hati za
hakimiliki hakuna mtu anayeweza kuwapokonya kirahisi."