Mgombea wa urais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma leo, akiendelea na kampeni zake za kuisaka Ikulu
nchini Kote huku akiwaomba Watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba
25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze
kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.PICHA NA MICHUZI
JR-DODOMA
Akitoa hotuba yake katika moja ya mikutano yake
alioufanya katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli amesema hakuna
kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea kati ya
wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto mkoani
Manyara.
Dkt Magufuli ameahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa na
kuunda Serikali yake,jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa
umakini mkubwa. “Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri na watendaji wengine
wa serikali halafu Mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo , Mkuu wa
wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo,
wamiliki wa Ng’ombe wabaki wanakula maisha haiwezekani,nitalala nao
mbele na Ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe
waliousababisha”,alisema Magufuli kwa msisitizo mkubwa.
Magufuli amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani
bila kubaguana, lakini pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha
maeneo ya wafugaji na wakulima yanatengwa, ili
wafanye shughuli zao na kukuza kipato na uchumi wao
bila kusumbuliwa.
Baadhi ya wananchi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake
wakimsiiliza Dkt Magufuli alipokuwa akinadi sera zake za kuomba kura ili
kushika nafasi ya Urais ya
awamu ya tano.
Waziri Mkuu wa zamani, Jaji
Mstaafu Joseph Warioba, akimnadi Dkt.Magufuli kwa kuhubiri amani katika
mikitano yake ya kampeni kuliko wagombea wa vyama vingine hawasisitizi
kudumisha amani nchini jambo ambalo ni tunu ya
taiafa
Dkt. Magufuli akimnadi
mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi
ya CCM, Ndugu Anthony Mavunde wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa
Jamhuri mjni Dodoma leo.
Dk Magufuli akimnadi Mgombea
ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje,mjini MPwapwa katika uwanja wa
mgambo.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge
Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa
kampeni jimboni humo.
Mawaziri wakuu wa zamani, John
Samuel Malecela na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba wakifuatilia
mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa
Dodoma kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea urais wa
Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, akimsimamia Mgombea ubunge Jimbo la
Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde aliyekuwa akifanya mazoezi ya Push
Up wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dodoma, Adam Kimbisa akimuombea kura Dk Magufuli wakati wa mkutano
huo wa kampeni mjini Dodoma jioni ya leo.
Walemavu nao wana haki ya kuwasikiliza Wagombea nafasi
mbalimbali ikiwemo ya Urais,Ubunge na Udiwani
Wananchi wa Kibaigwa wilayani
Kongwa, wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt. Magufuli alipokuwa
akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini
Kongwa.
Mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo
na Waziri Mkuu wa zamani Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba,mjini Kibaigwa
wilayani Kongwa kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa wakifuatilia
hotuba za Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.
Dk Magufuli akijipigia kampeni
kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa leo.Akiwa wilayani Kongwa, Dk Magufuli amesema kuwa
akishinda urais atahakikisha anadhibiti mapigano kati ya wakulima na
wafugaji yanayoendelea nchini na kusababisha vifo vya watu
wengi
Dkt. Magufuli akiwapungia mikono
wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma
leo.