Mgombea wa jimbo la Simanjiro kwa tiketi ya CHADEMA ,James
Ole Milya
Na Woinde Shizza,Arusha
Licha ya uwepo wa madini ya Tanzanite katika wilaya ya
Simanjiro mkoani Manyara bado wilaya hiyo inakabiliwa na uhaba wa maji ,ubovu
wa miundombinu ya barabara pamoja na ukosefu
wa huduma za afya kwenye baadhi ya
vijiji .
Akizungumza katika mkutano wa Kampeni,Mgombea wa jimbo la Simanjiro kwa tiketi ya CHADEMA ,James
Ole Milya amesema kuwa iwapo UKAWA
wataingia madarakani watatunga sheria za kuhakikisha kuwa asilimia 50% ya
mapato yanayotokana na madini yatabaki nchini kuchochea maendeleo tofauti na
hali ilivyo sasa mchango wa madini kwa pato la taifa ni finyu
Mwenyekiti Mstaafu wa BAVICHA wilaya ya Arusha mjini,Noel
Olevaroya amesema kuwa kimama wa jamii ya kimasai wamekua wakipata shida
kutokana na matatizo ya ukosefu wa maji huku wakilazimika kutembea muda mrefu
kutafuta huduma hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kata ya Loibor-Siret David
Mollel amewataka Watanzania kujitokeza katika uchaguzi Octoba 25 mwaka huu
kwani uchaguzi huo utaamua hatma ya maisha ya watanzania na mustakabali wa
taifa kwa ujumla katika Nyanja za uchumi,siasa na kijamii.
Wilaya ya Simanjiro
ni wilaya inayokaliwa na wafugaji wa jamii ya wamasai ambao hutegemea
shughuli za ufugaji kwa kiasi kikubwa kama chanzo kikuu cha mapato mbali na
kilimo na shughuli za uchimbaji wa madini aina ya Tanzanite yanayopatikana
katika mji mdogo wa Mererani.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia