Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akiteta jambo na
Kamishna wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Vincent Msena
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao,
yamekamilika na kuwataka wananchi kufika katika vituo vya kupigia kura
siku nne kabla ya uchaguzi ili kuhakiki majina yao.
Mkurugenzi wa Uchaguzi
kutoka NEC, Bw. Ramadhan Kailima, aliyasema hayo jana wakati akizungumza
na Wahariri wa vyombo vya habari na kufafanua kuwa, wameandaa vituo
72,000 nchini kote ambacho kila kimoja kitakuwa na uwezo wa kuhudumia
watu 450.
Alisema uandikishaji
wapigakura kwenye Daftali la Kudumu umefanyika kikamilifu kwa kutumia
mfumo mpya wa BVR ambapo hadi sasa, watu milioni 23 wameandikishwa na
idadi kamili itatolewa wiki ijayo.
"Siku ya kupigakura
vituo vitakuwa wazi kuanzia saa moja asubuhi na kufungwa saa 12
jioni...wapigakura hawaruhusiwi kubaki kwenye vituobaada ya kupigakura
ili kuondoa malumbano yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani," alisema Bw.
Kailima.
Aliongeza kuwa, majimbo
ya uchaguzi yako 264, kata 3,957 ambazozitashiriki uchaguzi na NEC
ndiyo yenye dhamana ya kutangaza matokeobaada ya kubandikwa kwenye vituo
vya kupigia kura na kuhakikiwa.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema katika baadhi ya
majimbo na kata, uchaguzi umesitishwa kutokana na vifo vya wagombea
wabunge, madiwani.
Majimbo hayo ni Lushoto
(Tanga), Ulanga Mashariki (Morogoro) na udiwani Kata za Bomang'ombe,
Bukene, Msingi Mkalama, Muleba na Uyola ambayo uteuzi wa wagombea wake
utafanyika Oktoba 12, kampeni zitaanza Oktoba 13 hadi Novemba 18, mwaka
huu na kura zitapigwa Novemba 22, mwaka huu," alisema.