Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha
Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya
taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu
Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi wakati
wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akiteta jambo na
Kamishna wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Vincent Msena wakati wa mkutano
baina ya NEC na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu nchini
uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa
Pwani Hussein Kibindu akisoma taarifa ya mada ya tathimini ya uchaguzi
mkuu wa oktoba 25 mwaka huu wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu
wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa
Mwanza, Alfred Kapole akichangia mada wakati wa mkutano mkutano baina ya
taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkalimani
wa lugha ya alama, Kudra Munishi akitoa ufafanuzi wa mada na hoja kwa
watu wenye ulemavu wa kusikia wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu
wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA).
Na Ismail Ngayonga MAELEZO
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitoa wasiwasi vyama vya siasa kuwa
hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi
wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25
Oktoba, mwaka huu.
AIdha
NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika
kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo
kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.
Hayo
yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na
wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya
kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi
oktoba mwaka huu.
Jaji
Lubuva alisema hadi kufikia sasa, vyama vyote vyote vinavyoshiriki
uchaguzi huo vimefanyika kampeni za kistaarabu ingawa katika siku za
hivi karibuni baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa kauli na matamshi
yaliyovuka mipaka, ambapo NEC imevionya vyama kuacha mara moja tabia
hiyo.
“Vipo
baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao wamekuwa wakitumia muda
mwingi kutoa lugha zisizofaa baada ya kunadi sera ya vyama vyao, vyama
hivyo tumekutana nao na kuwataka kuacha mara moja kampeni za aina hiyo”
alisema Jaji Lubuva.
Jaji
Lubuva alisema tarehe 27 Julai mwaka huu, vyama vyote vya siasa
vinavyoshiriki uchaguzi mkuu vilisaini maktaba wa maadili ya uchaguzi
huo, hivyo ni wajibu wa vyama hivyo kuzingatia viapo walivyotoa katika
maktaba huo.
Akifafanua
zaidi Jaji Lubuva alisema iwapo chama chochote hakina hoja ya
kuzungumza na wananchi ni vyema kikawa kimya hadi siku ya uchaguzi
tarehe 25 Oktoba mwaka huu.
Aidha
Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuingilia masuala
ya utawala ya tume hiyo, kwani kwa kufanya hivyo vyama hivyo vitakuwa
vikifanya kazi za tume hiyo na hivyo kuingilia masuala ya ndani ya
kiutendaji ya taasisi hiyo.
Akizungumzia
maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Lubuva alisema mahitaji yote ya msingi
ya uchaguzi huo tayari yamepokelewa na NEC ikiwa karatasi, wino, na
masanduku ya kura ambapo baadhi yake yameanza kusafirishwa katika maeneo
mbalimbali nchini.
Kuhusu
Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva alisema katika kipindi
cha siku 10 zijazo kuanzia sasa Tume hiyo inatarajia kusambaza daftari
la kudumu katika mikoa yote nchini na wananchi watatakiwa kuhakiki
majina yao katika kipindi cha siku 8.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia