NDEGE ya mafunzo ya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imepata ajali ikiwa na
marubani wawili katika eneo la Silversands, Visiwa vya Bundya, katika
Mwambao wa Bahari ya Hindi Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Dar es
Salaam.
Taarifa iliyotolewa
jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi, Upanga,
ilisema marubani hao wanaendelea kutafutwa baada ya kuzama habarini.
Tukio hilo limetokea
Oktoba mosi, mwaka huu, saa tatu 3:30 asubuhi ambapo marubani waliopotea
ni Luteni Kanali Talkisiyo Ndongoro na Kapteni Gaudence Hamis.
Chanzo cha ajali hiyo
ni hitilafu ya injini ambapo baada ya marubani kugundua hitilafu hiyo,
walifanya juhudi za kujiokoa kwa kutoka katika ndege, kuangukia baharini
na kuzama.
CHANZO: MAJIRA