Wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki wakiwa katika mstaari kwaajili ya kupiga kura hii leo
Na Woinde Shizza,Arusha
Baadhi ya wananchi wa
jimbo la Arumeru mashariki wamepongeza
tume ya uchaguzi kwa jinsi walivyofanya
maandalizi ya siku hii ya kupiga kura jambo kuna changamoto chache
zilizojitokeza.
Hayo wamebainisha leo wakati walipokuwa wakiongea mwandishi
wa habari hizi kusema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi kwa mwaka huu wamejitaidi
kuboresha huduma zao kuanzia katika daftar I la kudumu la kupiga kura
pamoja na jinsi ya wananchi wanavyopiga kura.
Mmoja wa mwananchi ambaya alikuwa akipiga kura katika kituo
cha Ngateu kilichopo katika kata ya Kiranyi ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki
Pelaji
Massae alisema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wakipee na utaweka historia
kwa nchini na kwa mataifa kwa ujumla.
Alisema kuwa katika uchaguzi huu wananchi wengi wameamka
mpaka sehemu za vijijini wametambua maana halisi ya siasa,wamejua faida za
kupiga kura na kumchagua kiongozi atakae muongoza na atake mletea maendeleo.
Naye mwananchi mwingine wa kituo cha Sakina Lomayani Laizer alisema kuwa amefurahi kuona vijana wengi ,pamoja na
wanaume wengi wamejitokeza kwa wingi
kupiga kura na hii ni dalili
inaonyesha kuwa wananchi wametambua
jinsi ya kutumia haki yao ya msingi ,pamoja na faida ya kumchagua
kiongozi wanaemtaka.
Alisema kuwa pia katika kipindi hichi swala la rushwa
limepungua kwani wananchi wengi wamejua faida ya kuchagua kiongozi bora na kuchagua kiongozi bila ya kupewa rushwa ya
aina yeyote.
“kweli Rushwa katika kipindi hichi haina nafasi na hajawahi
kuonekana tangu kipindi cha kampeni kianze na watu wameelimika kupita kiasi”
alisema Raimondi kibori
Naye Rehema bakari alisema kuwa anapenda kuwasihi jinsi
walivyoweza kutulivu katika kipindi cha kampeni
pamoja na leo katika kupiga kura ndio watulie ivyo ivyo katika kipindi cha kupokea
matokeo ili inchi yetu iendelee kuwa katika histoa ya nchi yenye amani pamoja
na utulivu.
Mwandishi huyu aliweza kushuhudia mamia ya watu wakijitokeza
kupiga kura kwa utulivu huku maeneo mbalimbali ya mkoa huu yakiwa na utulivu tofauti na siku
nyine ,sanjari na kushuhudia jeshi la polisi wakiendelea kulinda amani.