WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUKATAA MIHEMKO YA VYAMA KAMPENI ZA UCHAGUZI ZINAZOENDELEA

Mbunge viti maalumu kupitia Wazazi Phide Mwakitalima ambaye naye aliongozana na vijana hao katika kuhamasisha kumchagua kiongozi anaefaa kuongoza jiji la Arusha na kuleta maendeleo

 
Mbunge wa viti maalumu Phide mwakitalima akiwa anamuamasisha mmoja wa mfanyabishara kuchagua kiongozi anaefaa siju ya october 25

habari picha na woinde shizza,Arusha
Wananchi wa mkoa wa Arusha na vitongoji vyake wametakiwa  kukataa  mihemko  ya kampeni za uchaguzi  ili  isiwe chanzo cha  kuwagawa na kuwagombanisha wao kwa wao kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya vijana kutoka katika vyama mbalimbali vya siasa mkoani  Arusha wakati walipokutana kuzungumzia hatma ya jimbo lao la Arusha mjini .

walisema kuwa kwa mkoa wa arusha kumekuwa na mhemko ya siasa ambayo imewatawala sana vijana hali ambayo inapelekea uvunjifu wa amani na hata kuleta ugomvi .

Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Sauli Melayeki ambaye alitokea katika kata ya Olasiti alisema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi  kuachana na miemkoa ya kisiasa na kutambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.

Alisema kuwa imefikia wakati vijana kukaa chini na kutafakari na kufanya siasa zamsingi na kuacha siasa za ushabiki ambapo zinapekea kuchagua kiongozi mradi kiongozi bila hata ya kumuangalia kama ana faa au hafai.

Alisema kuwa kwa kipindi hichi wananchi wa jiji la arusha wanatakiwa wakae chini wafanye tasimini wawaangalie viongozi wote kutoka vyama vyote ambao wanagombania nafasi mbalimbali za uongoz i wakianzia wabunge pamoja na madiwani wao waaangalie uelewa wao au kama watafakuwaongoza na kuweza kukuwawakilisha vyema wananachi wao katika sehemu husika na sio wale viongozi ambao watakuwa wanasababisha uvunjifu wa amani.

kwaupande wa kijana mungine aliyejitambulisha kwa jina la Anna Mwambapa alisema kuwa wananchi wajitaidi kufanya siasa za amani zisizoleta chuki ,machafuko pamoja na uvunjifu wa amani na iwapo vitu hivyo vitatokea basi wamama na watoto pamoja na wananchi kwa ujumla watapata shida sana.

Aidha alibainisha kuwa mkoa wa huu na jiji kwa ujumla umepoteza muelekeo kabisa katika kipindi kilichopita kwani kiongozi waliomchagua akuwa muadilifu akutekeleza ahadi yeyote ambayo aliwahaidi hususa ni wao kama wafanya biashara na badala yake amesababisha wao kama wafanyabiashara kunyanyanyasika pamoja na kuteseka kwani aliwahaidi kuwatengea sehemu ya kufanyia biashara lakaini ajafanya hivyo adi sasa wamekeuea wakifukuzwa kila siku kama wakimbizi.

"mimi naomba tuwe makini sana kuchagua kiongozi katika kipindi hichi na tusifanye kosa kama kipindi cha nyuma tulivyofanya kosa kwa kumchagua mtua ambaye kila siku amekuwa anafanya maandamano alituahadi wafanyabiashara mengi lakini amna ata moja alilolitekeleza badala yake amekuwa ni mtua ambaye atumuelewei "alisema Mwambapa

Aliongeza kuwa ni wakati  wa kila mwananchi kumchagua kiongozi ambaye anafaa kiongozi ambaye anania na kiongozi ambaye anawajali wananchi wake na yule ambaye atawathamini kwa kutekeleza ahadi ambazo  amewahaidi wananchi wake.


















 Vijana hao waliamua kutembelea pia soko la kwa morombo ili kuweza kuwahamasisha wafanyabiashara kuchagua kiongozi anaefaa siku ya tarehe 25


 baadhi ya vijana hao wakiwa wanaonyesha hisia zao
 pia kulikuwa na mechi walioiyandaa  yote haya yalikuwa ni kuamasisha kumchua kiongozi ambaye anaeweza kuibadilisha mkoa wa Arusha pamoja na kata zake
 hapa baadhi ya vijana waliamua kupiga push shap huku wakisema hapa kazi tu

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post