Mgombea wa Urais wa CCM Dk Shein Awahutubia Wananchi wa Mtambwe: Ahaidi Mwaka wake wa Kwanza Elimu ya Sekondari Bure: Matibabu ya Afya Nayo Bure katika Miaka Miwili ya Mwazo ya Uongozi Wake.

Kikundi cha Taarabu cha Kangagani Pemba cha Profesa Gogo kikitowa burudani wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, uliofanyika katika Jimbo la Mtambwe Kisiwani Pemba na kuhudhuriwa na Wananchi wengi. 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na viongozi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akiwasili katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika viwanja vya Makoongeni Mtambwe Pemba.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiwapungia mkono Wananchi wa Kijiji cha Mtambwe alipowasili katika viwanja hivyo kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mtambwe wakiwa na mabango yenye ujumbe huo wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Kisiwani Pemba. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Merwa Hamad Mberwa wakati akiwasili katika viwanja vya mkutano vya Makoongeni Mtambwe kuendelea na mikutano yake ya kampeni kisiwani Pemba.
Wanachama wa CCM Pemba wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Makoongeni kwa ajili ya mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mtambwe Pemba na kuhudhuriwa na Wananchi wengi wa maeneo hayo ya mtambwe.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wete Pemba Kombo Hamad akitowa salamu za WanaCCM wa Wilaya yake wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na kuwataka Wananchi kumpigia Kura Dk Shein, kuzidi kuleta maendeleo kwa Visiwa vya Unguja na Pemba. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mtambwe na kutowa Sifa za Mgombea wa CCM Dk Shein, kwamba ni Mchapa Kazi na Uongozi wake Imara kwa Maendeleo ya Wazanzibar ili kuijenga Zanzibar Mpya katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka mitano ijaya. ili kuendeleza adhima yake ya maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar.
 Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM wakati wa mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya makoongeni mtambwe Pemba.
Mjumbe wa Malmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Karume akiwataka wananchi wa Jimbo la Mtambwe kumpigia Kura ya Ndio Dk Shein, ili kumchagua kuiongoza Zanzibar kwa maendeleo na kusema Uchaguzi sio kitu cha kujaribu   
Kada wa CCM Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Wananchi wa Mtambwe wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya makoongeni, amewataka Wanawake wa Mtambwe kuwaelimisha Kina Baba jinsi ya mafanikio ya CCM kwa kuipigia kura CCM ili kuendeleza wimbi la nmaendeleo katika kisiwa cha Pemba katika sekta mbalimbali za Uchumi CCM ndio chama pekee kinacholeta amani na upendo kwa wananchi wake.
Wanachama wa CCM wakimshangilia Balozi Amina Salum Ali wakati akihutubia katika mkutano huo wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein uliofanyika katika jimbo la Mtambwe Pemba. 
Kada wa CCM Dk Sira Ubwa Mwaboya akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mtambwe na kuwataka kukipigia kura CCM kwa maendeleo ya Wazanzibar na kusema Mtambwe ya sasa siyo ile ya zamani  imekuwa na mabadiliko makubwa katika kipindi cha miaka ya sasa katika sekta zote za maendeleo kwa wananchi wake.
Wananchi wa Jimbo la Mtambwe wakiwa katika viwanja vya Mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakisikiliza sera za CCM kwa miaka mitano ijayo dhidi ya Uongozi wa Dk Shein. 
Mkalimani wa Lugha za Alama kwa Watu wasionikia akitowa ishara kwa vitendo kutowa ujumbe wa Watu wenye mahitaji maalum waliohudhuria katika mkutano wa kampeni ya mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Sheim Jimbo la Mtambwe.
Balozo Seif Ali Iddi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mtambwe wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Shein, uliofanyika viwanja vya makoongeni mtambwe na kuwataka kukipigia kura Chama cha Mapinduzi ili kumchagua Dk Shein kwa Maendeleo ya Zanzibar kutimiza ahadi za Ilani ya CCM kwa kipindi chake cha Pili cha Uongozi wake. 
Wanachama wa CCM Jimbo la Tambawe wakimshangilia Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwahutubia katika mkutano wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Mberwa Hamad Mberwa akiwahutubia wananchi na kutoa historia ya iliokuwa mtambwe ya zamani hadi mafanikio yaliopatika kwa sasa kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, kuwahutubia Wananchi hao.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mtambwe wakati wa mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba uliofanyika katika viwanja vya makoongeni mtambwe na kuhudhuria na wananchi wengi wa jimbo hilo. 
 Wananchi wa Mtambwe Pemba wakimsikiliza Dk Shein, wakati akiwahutubia na kuomba kura kwa wananchi hao ili kuleta maendeleo kwa Wanamtambwe katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Wanachama wa CCM wakimsikili Mgombea Urais wa CCM Dk Shein, akiwahutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mtambwe katika mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba uliofanuika viwanja vya makoongeni na kutoa ahadi katika kipindi chake cha Pili cha Urais wa Zanzibar, akiingia madarakani mwaka wake wa kwanza Elimu ya Sekondari itakuwa bure na miaka miwili ya Uongozi wake Matatibabu Zanzibar yatakuwa Bure kwa Wananchi wa Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakimsikili Mgombea Urais wa CCM Dk Shein, akiwahutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Vijana wa Jimbo la Mtambwe wakifuatilia hutuba ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Shein wakati wa mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni mtambwe Pemba.

Wanachama wa CCM wakimsikili Mgombea Urais wa CCM Dk Shein, akiwahutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Ubunge wa Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofafanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wa Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofafanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Udiwani wa Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofafanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM wakiitikia dua baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni ya kugombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba.
Imetayarisha na OthmanMapara.Blogspot. zanzinews.com
Email othmanmaulid@gmail.com
Mobile No 0777424152 Or 0715424152.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post