HAYA NDIO MANENO AMBAYO MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA MOSHI MJINI ALIYOMWAMBIA NDESAMBURO

MH. Mwita Mchumi wa ccm Wilaya ya Moshi mjini na Meneja Kampeni wa Mgombea Ubunge wa Moshi Mjini akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya njoro.


Mgombea ubung  kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha Amwambia Mbunge Mstaafu wa Moshi Mjini kupitia Tiketi ya Chadema Mh. Philemon Ndesamburo awaambie wanachama wa chama hicho ukweli kuhusu Utendaji kazi wake.



Mh. Davis Elisa Mosha akisisitiza jambo kwa Mamia ya wakazi wa kata ya njoro


Mh Davis Mosha ameyasema hayo leo katika Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani katika kata ya Njoro, Mh. Davis Mosha akizungumza na Umati wa wananchi wa Kata hiyo ya Njoro alisema Anamuheshimu sana Mzee Ndesamburo ka Kazi aliyoifanya katika kipindi alichokua na Hana shaka katika hilo na anajua fika Mzee Ndesamburo anajua Utendaji wake wa Kazi.”Mzee Ndesamburo anajua mimi ni Mpambanaji, na anajua fika kuwa mimi ndiye iongozi sahihi ninayeweza kuwavusha kutoka hapa alipowaanha mpaka kwnye maendeleo. Nawatuma nendeni kamwambieni kuwa asikae kimya kama ana mapenzi ya dhati na Moshi mjini basi awaambie kuhusu mimi na afute kauli ya kurithisha jimbo kwa mtu ambaye anaamini bado hana uwezo wa kuliongoza hili Jimbo.” Alisema Mh. Davis Mosha huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi.

Mh. Davis Mosha Akiwapa nafasi wananchi wa Njoro kusema changamoto zinazowakabili.


Hata hivyo Mh. Davis Mosha hakuacha kueleza wananchi juu ya utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa moshi ikiwemo Ajira kwa vijana, Afya, Elimu na Hali ya Ulinzi na Usalama wa Moshi. Davis Mosha aliwaambia wakazi wa Njoro kumchagua kwa kishindo Diwani wa Kata hiyo Ndugu Zuberi na kuongeza kuwa ni mchapakazi na ataweza kufanya nae kazi kwa usahihi. Pia aliwaomba kuhamasisha ndugu zao na wakazi wa kata mbalimbali kuwachagua madiwani wa Chama cha Mapinduzi na katika kura ya Urais Mh. Magufuli anatosha na katika Ubunge hapo si pakufanya makosa ni Davis elisa Mosha.
Mkutano huo uliisha ka maandamano makubwa yaliyokua yakimsindikiza Mh. Davis Mosha wakati anatoka katika viwanja vya Relway eneo ambalo ulifanyika mkutano huo.

Mamia ya wakazi wa Moshi wakimsikiliza Mgombea Ubunge Moshi mjini Mh. Davis Mosha

Mh. Davis Mosha akinadi Sera za chama cha Mapinduzi kwa wananchi wa Njoro
Mgombea Udiwani kata ya Njoro Mh. Zuberi akitoa salamu ya ccm kwa wakazi wa Njoro.


Wananchi wa Njoro wakiwa wamembeba Mh. Davis Mosha baada ya Kuisha kwa Mkutano

Umati wa wakazi wa Njoro ukisindikiza Gari alilopanda Mh. Davis Mosha baada ya Mkutano kumalizika.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post