Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo. |
Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio. |
Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge . |
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo. |
Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia. |
Wengine walitishia kujinyonga mbele yake. |
Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge. |
Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea. |
Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio. |