Mamlaka ya
usajili wa vitambulisho vya Taifa(NIDA) imekamilisha zoezi kwa asilimia 93.3%
kuandikisha na kutoa vitambulisho kwa wafayakazi wa sekta ya umma mkoani Arusha
ambapo jumla ya wafanyakazi 26,992 toka kada mbali mbali serikalini
walitarajiwa kuandikishwa katika zoezi hili ni 25,278 ndio wameandikishwa na
kupewa vitambulisho huku wengine wakishindwa kujiandikishwa kutokana na sababu
mbalimbali
Akisoma
Taarifa hiyo wakati akipokea vitambulisho hivyo vya watumishi wa serikali
mkoani hapa ofisini kwake Katibu Tawala wa mkoa Huo Richard Kwitega alisema
kuwa changamoto kubwa waliokumbana nayo ni kuchelewa kujitokeza kwa baadhi ya
watumishi ambao walikuwa wakichanganya zoezi hilo na zoezi la kuhakiki vyetu.
Kwitega
alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo bado zoezi hilo halikuweza kuathirika
ambapo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye
zoezi linalotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa
Januari,
Alisema kuwa
jumla ya makadirio ya wananchi wanatarajiwa kuandikishwa kwenye zoezi hilo kwa
kuchukuliwa taarifa zao ni 975,988 ambap kwa siku wanatarajia kuandikiasha watu
50 kwa mwandikishaji moja ili kupunguza misongamano.
Akavitaka
vyombo vya habari,viongozi wa umma, kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya
umuhimu wa vitambulisho vya taifa ili siku ya kuanza kwa zoezi hilo waweze
kujitokeza kwa wingi nakuweza kutumia fursa hiyo.
Alisema
ushirikiano wa serikali na Nida ndio umeweza kufanikisha zoezi hilo kwa
watumishi wa umma ambapo ambao hawajajiandikisha walitokana na wengine kuwa
masomoni na wagonjwa ambapo kwa sasa watawafata huko walipo ili waweze
kuwaandikisha wote.
Nae Afisa
usajili wa Nida mkoa wa Arusha Julieth Raymond Mwacha alisema kuwa zoezi hilo
limeenda vizuri na kuwataka wananchi kusubiria zamu yao kwa kutoa taarifa zao
sahihi za kuomba kitambulisho cha taifa kwani zoezi hilo hivi karibu litaingia
kwa wananchi wa mkoa mzima.
Alisema kuwa
zoezi hilo likikamilika litaisaida serikali hata kwenye takwimu zake mbali
mbali kwani taarifa zimewekwa kwenye kanzidatam na kukoa fedha ambazo
zingetumika katika mazoezi mengine ya kitakwimu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia