Mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema wamefikishwa katika
mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha kusomewa mashtaka yanayowakibili
katika kesi namba 351 ambapo wanatuhumiwa kutuma meseji yenye ujumbe wa
kumtukuna mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo
Wakili
wa upande wa mashtaka Alice Mtenga amewataja mashahidi watano
wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambao watatoa
ushahidi katika kesi hii
Hata
hivyo mawakili upande wa utetezi wakiongozwa na John Malya umetoa
notisi ya pingamizi la awali la mdomo kuwa hati ya mashitaka ina
mapungufu kwa hiyo baadae wataiomba mahakama itupilie mbali hati hiyo.
Hakimu anayesikiliza shitaka hili Nestory Barro ameiahrisha kesi hiyo hadi tareh 3 mwezi februari mwaka huu