Na Woinde Shizza,Arusha
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amelazimika
kurudishwa tena gerezani mara baada ya Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha kushindwa kutoa uamuzi baada ya upande wa Jamhuri kukata
rufaa kwenda Mahakama ya Rufani kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.
Jaji wa Mahakama kuu ya Arusha aliyekuwa akisikiliza
kesi hiyo Salma Magimbi ameshindwa kutoa
maamuzi kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa ya mahakama kuu ya Rufaa
kupinga dhamana dhidi ya Mh. Lema.
Jaji huyo amesema hana mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo
kutokana na uamuzi huo; hivyo kusababisha mbunge Lema kurudishwa tena mahabusu.
Kwa upande wa Wakili mtetezi wa Mbunge Lema John Malya
akielezea mwenendo wa kesi hiyo kwa niaba ya mawakili wenzake amesema
wamesikitishwa na uamuzi uliotolewa mahakamani leo kwani Jamhuri wangepaswa
kutoa uamuzi wa dhamana na siyo kukata rufaa juu ya rufaa.
Amesema jambo hilo linalobishaniwa na upande wa Jamhuri
lipo wazi na kwamba wanajipanga kwenda katika mahakama kuu ya rufaa kabla yao
ili shauri hilo liweze kusikilizwa na mteja wao amekubaliana nao.
Mbunge huyo amerudishwa tena Rumande hadi hapo kesi hiyo
itakaposikilizwa tena ambapo mpaka sasa amefikisha siku 61 akiwa mahabusu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia