ZAIDI YA WAKULIMA 60,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA( AMDT)


Pichan ni  Martin Mgallah ambaye ni Meneja mradi wa Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania (AMDT)Picha na Vero Ign atus Blog 27januari2017.

Wakwanza kushoto ni akiyevaa tshirt nyekundu ni Hellen Wakuganda kutoka Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo(PASS)akifuatiwa na aliyepo katikati Al-Amani Mutarubukwa kutoka (AMDT)akifuatiwa na Juliana Nganyangwa kutoka (AMDT)wakitoa elimu kwa wakulima Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.27 january 2017.


Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania (AMDT)imewataka wakulima kubadilisha kilimo kuwa biashara ,waondokane na kilimo cha kawaida na kuwa na kilimo cha kisasa na kufahamu kilimo mkataba.

Hayo yamesemwa na meneja mradi Martin Mgallah alipokuwa katika maonyesho ya zana za kilimo Jijini Arusha na kusema kuwa wametenga zaidi ya dola za kimarekani milioni kumi na tano kwaajili ya kuwawezesha wakulima katika zao la Alizeti pekee ndani ya  miaka mitano (2016-2021)

“Taasisi itamuwezesha mkulima kuongeza kipato chake cha mwaka kwa kubadilisha kilimo kuwa biashara,tunaangalia pia mfumo wa masoko,tunamuwezesha mkulima kufahamu kilimo mkataba yaani akishalima na kuvuna mazao yake asihangaike tena kutafuta soko bali atauza mazao yake kwa bei nzuri,tunamuunganisha na soko moja kwa moja”alisema meneja mradi Martin. 

Amesema kuwa wakulima zaidi ya 60,000 watanufaika na mradi huo,huku akianisha mikoa ambayo wataanza nayo ambayo ni pamoja na Manyara,Shinyanga,Singida,Dodoma,Iringa,Njombe,Mbeya Songwe ,Katavi,Lindi,Rukwa na Mtwara.

Martin amesema kuwa lengo kubwa la( AMDT) kuhakikisha kuwa mkulima anazalisha kilicho bora ,amesema mazao ambayo wataanza nayo ni Alizeti,mahindi,na jamii ya mikundekunde katika mikoa tajwa.


Aidha amesema kwaba wanampatia mkulima elimu sahihi,namna ya kulima kilimo cha kisasa,kumuelimisha mkulima  kuwa na bima itakayomuwezesha kupata nyezo za kisasa za kilimo hivyo amewataka wakulima kuwatembelea ili waone ni kwa namna gani wanaweza kunufaika na program hii.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia