Naibu waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba ya ufunguzi wa
chilumbo, (kongamano) la Kiswahili, lililofadhiliwa na benki ya MCB, na
kufanyika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es
Salaam, Januari 27, 2017.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI
ya Mwalimu, (MCB), imetoa semina kwa walimu na washiriki wa Chilumbo,
(Kongamano), la Kiswahili lililofanyika Chuo Cha Mwalimu Nyerere Kigamboni
jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2017.
Katika
semina hiyo, maafisa wa MCB walielezea huduma mbalimbali zitolewazo na benki
hiyo mpya inayomilikiwa na chama cha walimu nchini, (TTU), ambapo Meneja
Mahusiano ya wateja wa benki hiyo, Bw.Charles Shadrack, (pichani juu),
alisema, benki hiyo
inatoa huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye riba
nafuu.
“Kwa
mfanyakazi wa serikali, anachotakiwa kuja nacho baada ya kufungua akaunti
kwenye benki yetu ni Salary sleep ambapo tunatoa mkopo wa hadi shilingi
milioni
30.” Alisema.
Alisema,
benki hiyo pia imo kwenye kundi la mabenki yanayotumia ATM za umoja hivyo
mteja
anayo fursa ya kupata huduma za kibenki mahala popote nchini.
Akifungua
chilumbo hilo, Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.
Anastazuia Wambura, amewataka washiriki kukienzi Kiswahili kwani ni lugha
inayokua kwa kasi duniani.
“Rais
wetu ameonyesha njia, niwape changamoto magwiji wa Kiswahili, jifunzeni kwa
bidii ili mkitumie kama ajira kwani soko la walimu wa Kiswahili linapanuka
siku
hadi siku.” Aisema.
Wasiriki wakifurahia mada zilizokuwa
zikitolewa
Washiriki wakiwa kwenye ukumbi wa
Utamaduni palikofanyika chilumbo
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, (kushoto), akipena mikono na
Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, mara baada ya kutoa
hotuba yake
Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB,
Rahma Ngassa, Meneja wa Huduma kwa wateja wa benki hiyo, Bi.Flora Mbogo na
Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, wakiwasikiliza washiriki
mbalimbali waliohudhuria chilumbo (kongamano), hilo na wakataka kujua
huduma zitolewazo na MCB
Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles
Shadrack,(kushoto), akifafanua jambo kwa washiriki hawa waliokuwa na kiu ya
kujua huduma zitolewazo na benki hiyo mpya kabisa hapa nchini
Meneja wa MCB, tawi la Samora
katikati ya jiji, Bw.Cassian Clovis, (kushoto), akijadiliana jambo na
Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, na Afisa Mikopo wa benki
hiyo, Bw.Isaya Hagamu, huku chilumbo kikiendelea
Wimbo wa taifa ukiimbwa
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere, anayeshughulikia masuala ya Mipango, Fedha na Utawala,
Dkt.Magreth Shiwa, akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni
Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki hiyo. |
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba |
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa
makini
Msanii Muhogo mchungu naye alikuwepo
kwenye chilumbo (kongamano) la Kiswahili
Afisa Mikopo wa benki ya MCB,
Bw.Isaya Hagamu, (wakwanza kushoto), akitoa maelezo ya shughuli zifanywazo
na benki hiyo kwa washiriki hawa waliokuwa na hamu ya kutaka kujua huduma
zitolewazo na benki hyo
Afisa Mikopo wa benki ya MCB,
Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki
hiyo.
Mtunzi maarufu wa vitabu Shafi Adam
Shafi naye alikuwepo
Meneja Masoko na Uhusioano wa MCB,
Bi. Rahma Ngassa, (katikati), na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw. Charles
Shadrack, (kushoto), wakimsikiliza mwenyeji wao Meneja Uhusioano wa Chuo
Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Bi. Evelyn Mpasha
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia