Usiku wa 31,December 2016 kuamkia mwaka mpya
2017 ndipo wanamitindo mbalimbali walikutana na kusherekea kwa pamoja Usiku wa
Khanga yaani “Khanga Party”. Tukio hili kama lilivyo kuwa limetaarifiwa awali
limefanyika Regency Park Hotel. Design mbalimbali za vazi la Khanga kutoka
kwa wanamitindo zilioneshwa kwenye stage na kuzikonga mioyo za wadau pamoja na
wahudhuriaji usiku huo.
Kumbuka
Party hii imeandaliwa na Mama wa Mtindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, mbali
na burudani zilizo kuwepo pia kulikuwa na Red Carpet yenye sifa kubwa ya kuwakutanisha
mastaa na mashabiki wao kuweza kupiga picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu.
Tunawatakia mwendelezo mwema na wenye baraka wadau na wanamitindo kutoka hapa
Tanzania. (Cheers 2017)