Na.Mwandishi Wetu,Chalinze
Serikali imesema haitasita kuaendelea kuhimiza na kuvutia
wawekezaji waaminifu, wenye mipango, dhamira na mikakati ya ujenzi wa
viwanda kwa nia ya kutanua wigo wa ajira na kukuza maendeleo ya
kiuchumi.
Msimamo huo.umetolewa jana na Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati akipongeza jitihada zinazofanywa
na mwekezaji wa kampuni TwyFord Tanzania Cereramics katika ujenzi wa
kiwanda cha kutengeneza vigae "Tiles" kilichopo Kijiji cha Pingo,
Chalinze Mkoani Pwani.
Waziri Mwijage alisema hayo mara baada ya kutembelea na
kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda cha
kutengeneza vigae kitakachozalisha ajira kwa watanzania zaidi ya elfu
mbili katika mfumo rasmi na ajira elfu nne zisizo rasmi.
“Kiwanda hiki kikikamilika kitasidia sio tu kutoa ajira
lakini pia kitawafanya watanzania kununua na kuuza bidhaa
zinazotengenezwa nyumbni badala kuangiza kila kitu kununua nje” Alisema
Mwijage.
Waziri huyo dhamana wa viwanda alisema, bidhaa hizo pia
zitauzwa katika nchi jirani kama Zambia, Malawi, DRC, Rwanda, Burundi,
Uganda na Jamhuri ya watu wa Afrika Kati pia kusafirishwa nje ya bara la
Afrika .
Aidha Waziri Mwijage alisema kuwa kiwanda hicho kitumike
vizuri hukubakitoa wito kwa watanzania kutumia fursa zitakazopatikana
katika mradi huo zitumike kwa faida ya kila mmoja.
“Serikali ya kijiji itambue maeneo yake ili kusaidia
kuharakisha maendeleo ya eneo hili mahali ambapo kiwanda kinafanya
shughuli zake”Alisema Mwijage.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete, alisema ujenzi wa kiwanda hicho kipo katika hatua ya mwanzo
ya Ujenzi na kinataraji kukamilika julai mwaka na kufunguliwa rasmi
Agosti mwaka huu.
Ridhiwani alisema kiwanda hicho kitasaidia kuufungua mji
wa Chalinze na kufanya uwe mji wa viwanda na biashara hivyo kutaanza
kufunguka kwa fursa za kiuchumi na kupanua mji huo sekta ya viawanda
katika juhudi za kuunga mkono serikali ya awamu ya tano.
“Ujenzi wa kiwanda hiki ni alama chanya ya jinsi serikali
ya awamu ya tano ilivyojidhatiti kufungua fursa za viwanda katika nchi
yetu.Wananchi wa Chalinze na mkoa wa Pwani nawaasa na kuwataka waendelee
kujipanga kwa nia ys kujenga viwanda ili fursa nyingi zaidi.”Alisema
Ridhiwani
Mbunge huyo wa chalinze alimshukuru mwekezaji wa kiwanda
hicho kwa kukubali kusaidia kumalizia ujenzi wa shule ya sekondari ya
kata ya Pera na kituo cha afya katika kata hiyo.
“licha ya kukubali kusaidia ujenzi wa huo lakini pia fursa
nyingine watu watapata nafasi ya kuuza mali ghafi zinazotumika
kutengeza vigae ambapo tunatarajia asilimia 90 malighafi hizo zitatoka
hapa kwetu katika mikoa ya jirani”.alisema Ridhiwan.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia