BREAKING NEWS

Monday, January 23, 2017

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MABILIONEA WAKUBWA DUNIANI

Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amepata nafasi ya kukutana na mabilionea wawili wakubwa duniani akiwa ziarani Davos nchini Uswisi.


Dr. JK ameshiriki katika uzinduzi wa baraza la kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 January 2016 huko Davos Uswisi ambapo baraza la kutokomeza Malaria linaundwa na Wajumbe 9 ambao ni watu mashuhuri katika sekta ya umma na sekta binafsi duniani na orodha yenyewe ya Wajumbe ndio hii hapa chini


1. Bill Gates – Mwanzilishi na mmiliki wa Bill Gates Foundation
2. Ray Chambers – Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria
3. Peter Chermin –Mwanzilishi wa Chermin Entertainment na Chermin Group
4. Aliko Dangote – Rais na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group
5. Idrisa Deby –Rais wa Chad kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taasisi ya ALMA
6. Jakaya Kikwete –Rais Mstaafu wa Tanzania
7. Graca Machel – Mwanzilishi wa Foundation for Community Development,Msumbiji
8. Luis Alberto Moreno –Rais wa Inter-American Development Bank
9. Ellen Johnson Sirleaf – Rais wa Liberia.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Bill Gates ambaye mpaka January 2017 jina lake limetajwa kuwa ndio anashika namba 1 kwa utajiri duniani


Lengo la Baraza hilo ni kuunganisha nguvu za wadau na mataifa duniani kukabiliana na hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030 ambapo kuanzishwa kwa Baraza hilo kumetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika vita dhidi ya malaria katika miaka 15 iliyopita.


Katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika Davos, Baraza hilo limejadili kuhusu upatikanaji wa rasilimali za kutosha za kuwezesha kutoa msukumo katika upatikanaji wa vifaa tiba, dawa, tafiti na uvumbuzi wa mbinu na nyenzo za kisasa za kuzuia, kupambana na hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Malaria katika nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini.

Jakaya Kikwete na Ray Chambers na Bill Gates
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Baraza hilo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye utotoni kwake alipoteza kaka yake kwa ugonjwa wa Malaria pamoja na ndugu wengine wengi katika maisha yake amesema, ” Kutokomeza Malaria iliwahi kuwa ndoto isiyotekeleza, lakini sasa kuifikia ndoto hiyo ni dhahiri…..tunawea kuifanya Malaria kuwa historia na kuutokomeza ugonjwa huu katili katika uso wa dunia”.


Tanzania ni moja ya nchi zinazosifika barani Afrika na duniani kwa kuweza kupiga hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya malaria yamepungua kwa asilimia 70 na vifo vimepungua kwa asilimia 50.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates