kamanda wa
polisi mkoani Arusha naibu kamishna wa polisi Charles mkumbo akiongea na waandishi wa habari hii leo juu ya uteketezaji wa magunia ya bangi ,pembeni ni mkuu wa kitengo cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Mihayo Msikhela
Na Woinde Shizza,Arusha
Jeshi
la polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na tume ya kuratibu na
kuthibiti dawa za kulevya nchini limeteketeza magunia 58 ya bangi,mbegu
za bangi kg 210 huku hekari 19 zilizooteshwa miche ya bangi zikiwa
zimeharibiwa .
Hayo yamebainishwa jana na kamanda wa
polisi mkoani Arusha naibu kamishna wa polisi Charles mkumbo wakati
akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa
kuteketeza kwa madawa haya ya kulevywa kumefanyika kutokana na
operationi ya siku mbili .
Alisema kuwa operesheni ya
kwanza ilofanyika january 10 siku ya jumanne kuanzia muda wa saa 11.00
alfajiri katika eneo la kijiji cha kisimiri juu ndani ya kata ya uwiro
tarafa ya kingori na kufanikiwa kupata magunia 31 pamoja na mbegu
kilogramu 210 ambazo zote ziliteketezwa na moto ,pamoja na hekari 19
zilizooteshwa miche ya bhangi ambazo ziliaribiwa zote.
Aliongeza
kuwa operationi hiyo iliendelea tena siku ya alhamisi january 12
kuanzia muda wa saa 11.00 alfajiri hadi saa saba mchana katika eneo la
kijiji cha Engalaon kata Mwandeti tarafa ya Muklati ambapo walikamata
jumla ya magunia 27 ya bangi na kuyateketeza na moto na kuharibu jumla
ya hekari 12 zilizooteshwa mmea wa bhangi .
Mkumbo
alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
usalama linaendelea na operationi hii hasa ya kuaribu mimea ya bangi
mara kwa mara hasa katika cha mvua hali ambayo itasaidia kuthibiti
kilimo hicho.
Aidha pia jeshi la polisi linawaonya
viongozi wa maeneo yanayohusika na kilimo cha bangi kuacha mara moja
kuwaunga mkono wakazi wa maeneo hayo kwani matukio hayo yanafanywa kwa
uwazi bila wao kuchukua hatua yeyote ,wanapaswa watambue kwamba wao ni
walinzi wa maeneo yao ,na kuwasihi viongozi washirikiane kwa pamoja
kutokomeza kilimo hicho cha bhangi ambayo inaleta madhara makubwa kwa
jamii.
kwa upande wake mkuu wa kitengo cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Mihayo Msikhela alisema kuwa mikoa ambayo inaongoza na kupatikana kwa zao la bangi ni Tarime ,Morogoro , Arusha pamoja na Kilimanjaro lakini kwa sasa viongozi waliopo katika sehemu hizo wanajitaidi sana kuthibiti ulimwaji wa mazao hayo ya bangi huku akichukuwa muda huo kumpongeza mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa kupiga vita ulimwanyi wa bangi pamoja na mkuu wa wilaya ya Tarime jinsi wanavyojitaidi kuthibiti ulimwaji huo wa bangi mpaka kufikia sehemu ya kuwaweza viongozi wa vijiji hivyo ndani kutokana na kusimamia ulimwaji wa zao hilo ambalo limepigwa marufuku hapa nchini
Aidha alisema kuwa kwakuwa tatizo hili limekuwa kama likijirudia wanampango wa kuboresha sheria za uthibiti ikiwa ni pamoja na kuweka sheria kali zitakazo wabana wale ambao wanatumia ,wanauza pamoja na wanao lima madawa haya ya kulevya hapa nchini .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia