Ticker

6/recent/ticker-posts

MAMIA WAMUAGA RUBANI NA MTENDAJI MSTAAFU WA WAKALA WA NDEGE ZA SERIKALI MAREHEMU KENAN MHAIKI



Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiaga mwili wa marehemu Kenan Mhaiki Rubani Mtendaji mstaafu wa wakala wa ndege za serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda Songea Mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4, Makaburi ya Matogoro. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogspot) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Leonard Chamriho akitoa salamu kwa niaba ya serikali wakati wa ibada ya misa na shughuli ya kumuaga Rubani na Mtendaji mkuu wa wakala wa ndege za serikali (TGFA) marehemu Kenan Paul Mhaiki shughuli iliyofanyika nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam Januari 2 2017.Mwili wa marehemu umesafirishwa jana na kwenda Songea mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo Januari 4 2017 kwenye makaburi ya Matogoro.
Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Ombeni Sefue akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kenani Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam jana. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kwenda Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4 2017. soma zaidi hapa

Post a Comment

0 Comments