Hatimaye
wananchi wa Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar waliojiandikisha katika
Daftari la Kudumu la Mpiga leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo
mbalimbali kupiga kura kumchagua Mbunge atakayewawakilisha kwa kipindi
cha miaka miaka 4.
Zoezi
la upigaji wa Kura katika vituo mbalimbali lilianza majira ya saa 1
asubuhi likifanyika kwa hali ya Amani na Utulivu huku baadhi ya
wananchi waliojitokeza kupiga kura wakipongeza maandalizi mazuri
yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzine (NEC) kufanikisha Uchaguzi
huo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage
akizungumza kuhusu mwenendo wa Uchaguzi huo mara baada ya kutembelea
vituo vya kupigia kura katika jimbo hilo na kuzungumza na Mawakala wa
Vyama vya Siasa waliokuwepo vituoni, Waangalizi wa Uchaguzi na
Wasimamizi wa Uchaguzi huo amesema Tume imeridhishwa na kazi nzuri
iliyokuwa ikiendelea katika vituo mbalimbali vya kupigia Kura.
Wananchi wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura katika kituo cha Bweleo katika jimbo la Dimani leo.
“
Viongozi wa Tume tumetembelea vituo mbalimbali vya kupigia Kura katika
jimbo la Dimani; tumeona wenyewe upigaji wa Kura unaendelea vizuri,
tumewauliza Mawakala, Watazamaji na Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi
kila mmoja amesema Uchaguzi unakwenda vizuri, nachoweza kuwaambia
watanzania Uchaguzi Dimani unakwenda Vizuri” Amesema Jaji Kaijage.
Amesema
Wasimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo hilo wanaendelea kufanya kazi zao
kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili pia kushughulikia kwa haraka
changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika baadhi ya vituo vya kupigia
Kura.
Ameeleza
kuwa zoezi zima la upigaji wa Kura linaendeshwa kwa uwazi mkubwa,
Utulivu na Amani na kuwawezesha wananchi kupiga kura bila vikwazo
vyovyote.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles
Kaijage (Katikati) akizungumza na Msimamizi kituo cha Dimani Bi. Abdu
Simai Haji leo wakati zoezi la upigaji kura likiendelea katika jimbo la
Dimani.
Aidha,
Mhe. Kaijage amebainisha kwamba endapo yatajitokeza malalamiko yoyote
wakati zoezi la upigaji wa Kura likiendelea katika vituo mbalimbali ,
Mawakala wa Vyama vya Siasa ambao ni wasimamizi wa Maslahi ya Wagombea
na Vyama vyao Vituoni watajaza fomu ya malalamiko Na. 14 kwa mujibu wa
Sheria ambayo inatoa fursa ya kushughulikiwa kwa malalamiko hayo.
Aidha,
amebainisha kuwa mara baada ya zoezi la upigaji wa kura kumalizika leo
saa 10 jioni kazi ya kuhesabu Kura itafuata ili hatimaye wamnanchi wa
Jimbo la Dimani waweze kupatiwa matokeo ya maamuzi waliyoyafanya kupitia
Kura zao.
Mhe.
Kaijage amesisitiza kuwa Wasimamizi wote wa Uchaguzi huo wamepewa
mafunzo ya kuzingatia ili kuhakikisha wanaendesha zoezi hilo kwa ufanisi
mkubwa na kuwezesha matokeo kutangazwa kwa wakati ili kuwawezesha
wananchi kumjua mshindi wa Uchaguzi huo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles
Kaijage (wa pili) akiwa ameambatana na Baadhi ya Watendaji wa NEC na
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Bi. Idaya Selemani Hamza (wa Kwanza)
akiwasili katika kituo cha Kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la
Dimani kuangalia maendeleo ya Upigaji wa Kura leo.
“
Endapo taratibu zote za Uchaguzi zitakuwa zimekamilika kwa mujibu wa
Sheria, hakutakuwa na sababu yoyote ya kuchelewesha matokeo,mpaka sasa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi tumeridhishwa na mwenendo mzima wa zoezi la
upigaji wa Kura na matokeo yatatolewa kwa wakati” Amesisitiza.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Bw. Emmanuel Kawishe akizungumzia zoezi la Upigaji wa Kura amesema kuwa
Wapiga Kura wanaoruhusiwa kupiga kura ni wale waliokidhi Sifa na Vigezo
vilivyoainishwa kisheria kuwawezesha kupiga Kura.
Amesema
kwa mujibu wa Sheria Msimamizi wa Kituo ndiye mwenye mamlaka ya
maamuzi katika kituo cha kupigia Kura ikiwa ni pamoja na kuamuru
kuondolewa kwa mtu yeyote atakayeonekana kufanya fujo au kuzuia zoezi la
uchaguzi kuendelea kituoni.
Katika
Uchaguzi Uchaguzi huo mdogo wa Ubunge wa jimbo la Dimani jumla ya
Wapiga Kura 9,280 wanatarajiwa Kupiga kura katika Vituo 29 huku vyama
vya Siasa vyenye wagombea vinavyoshiriki Uchaguzi huo ni 11 huku
Waangalizi wa Uchaguzi waliojitokeza kushiriki katika Uchaguzi huo ni
zaidi ya 300.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles
Kaijage (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa Zanzibar kutoa
tathmini ya hali ya Uchaguzi mara baada ya kuetembelea vituo mbalimbali
vya kupigia kura katika jimbo la Dimani leo.
Baadhi
ya Wangalizi wa Uchaguzi katika jimbo la Dimani wakifuatilia matukio
mbalimbali wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani
leo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles
Kaijage (Kushoto) akizungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo
ndani ya kituo cha kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani leo.
Wengine wanaochukua taarifa ni Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC).
Mmoja
wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge
katika jimbo la Dimani leo. Picha na Aron Msigwa –NEC.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia