Waislamu
wametakiwa kusomesha watoto wao ili kuweza kuendana na mifumo ya kielimu kwa
nyakati zilizopo na zijazo kwani vijana wa sasa wamekuwa na ulimwengu wa haraka
haraka na umekuwa unabadilisha lugha kila mara
Kauli hiyo
imetolewa na mjumbe wa baraza la ulamaa bakwata taifa sheikh Hassan chizenga
wakati akizungumza na waislamu kwenye uzinduzi wa ujenzi wa jengo la chuo cha
Al Azhar na mgeni Rasmi kuwa mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro
Sheikh
Chizenga alisema kuwa elimu ni kitu muhimu katika maisha na chuo hicho
kitakapokamilika watoto wetu watafundishwa kuijua dunia yao na akhera yao
itakayosaidia kuwa waadilifu katika utumishi wa umma na mbele ya muumba wao
kama mafundisho ya mtume Muhammad s.w.a.
Alisema kuwa
Kuijenga Tanzania yenye maadili mema amani na mshikamano inahitaji nguvu ya
ziada ya kuaandaa watoto wetu katika malezi mema ya kiroho na kidunia yatakayowasaidia
kupata fedha za halali na watoto wa halali ilikuweza kuendesha maisha ya halali
na hatimae watoto hawa kuwa waadilifu kwenye taifa lao.
“Tutambue
kuwa sisi tunaishi kwenye ulimwengu wenye kugeuka tabia kila mara na vijana
wetu wanazaliwa kwenye ulimwengu wa haraka haraka hivyo yatupasa kuwapa elimu
ya utambuzi itakayowasaidia kuishi maisha ya halali na kuja kulisaidia taifa
lao siku za usoni wakiwa waadilifu”alisisitiza Sheikh Chizenga
Aidha mgeni
rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
kwa niaba yake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alisema kuwa
taasisi za dini zimekuwa na mchango mkubwa kwa serikali hususani katika masuala
mbali mbali ya kijamii ikiwemo elimu na Afya.
Daqarro
alisema kuwa Taifa linahitaji kuwa na amani na mshikamano utakaosaidia
kuendelea kuwa darasa kwa mataifa yanaotuzungika na kuishi bila chuki na mtu
unaetofautiana nae mawazo kwa kukaa na kujadiliana nae tofauti zenu bila
munkari.
Alisema kuwa
viongozi wa serikali wanawategemea viongozi wa dini kuwajenga kiimani waumini
wao kujua umuhimu wa mafundisho ya kuitunza amani sanjari na uadilifu
utakalolisaidia taifa eltu kuendelea kuwa na amani na mshikamano kama hapo
mwanzo wakati wa waasisi wetu wa taifa hili.
“Amani ni
kila kitu amani ni sawa na Oxygen tuienzi kwani viongozi wa dini wamekuwa
washiriki wakubwa wa kuleta maendeleo katika nchi yetu kama nyinyi leo
mnavyoonyesha katika chuo hichi cha Al Azhar”alisema Daqarro.
Nae sheikh
wa mkoa wa Arusha Shaban Jumaa alisema jengo hilo litakapokamilika litakuwa na
ghorofa 14 na litagharimu zaidi ya billion 12 na litajengwa kwa awamu tatu
likiwa na lengo la kuboresha elimu ya dini na sekula pamoja na
hospitali,hosteli,shule ya awali,msingi hadi ngazi ya chuo.
Sheikh
Shaban alisema kuwa ujenzi wa chuo hicho utawashirikisha wanaarusha wote
kuchangia ujenzi wake,ambapo ukikamilika utazalisha vijana wenye maadili ya
kulitumikia taifa kwa uadilifu na uzalendo na uchungu kwa wananchi wanyonge.
“Nafikiri
amani imezungumzwa sana faida zake na hasara zake tuviangalie vyombo
tunavyoviongoza kwa jicho la utofauti kwa kuangalia mema ya mwenzako na
kuyazungumza huku mabaya mkikaa chini na kuyajadili mtafika kwenye kuheshimiana
nawasihi sana kuzungumza mema kuliko mabaya”alisema sheikh Jumaaa
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia