Nabii
mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini
walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo
Na Woinde Shizza,Arusha.
Watanzania
nchini wametakiwa kusaidia Jamii ya watu wasiojiweza ikiwemo walemavu,watoto
yatima pamoja na wazee ili waweze kupata mahitaji yao na kuondokana na umasikini
uliokithiri.
Hayo
yameelezwa na Baadhi ya Wananchi waishio katika kata ya Kisongo mkoani Arusha
ambapo walisema kuwa jamii ya wahitaji imekua ikiishi katika mazingira magumu
hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa anawasaidia jamii hiyo.
"katika
jamii kuna watu wengi wakiwemo watoto wanatoto na watu wasio jiweza
ambao wanakaa katika mazingira magumu mno hivyo ni wajibu wetu sisi
kuwasiaidia wale ambao awajiwezi ,mtu ukiwa na uwezao kidogo unatakiwa
ujijengee tabia ya kuwasiaida hawa wasio jiweza"alisema Sekela Tondolo
Kwa upande wake Mkazi mwingine wa kata ya
Kisongo Wiliam James Alisema kuwa jamii
ya wasiojiweza imekua ikisahaulika mara kwa mara hivyo ni jukumu la kila
Mwananchi kuhakikisha kuwa anafanya kitu kwa ajili ya jamii yake kitakacholeta
mchango ambao ni chanya na kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazokutana
nazo kimaisha.
Kwa upande
wake Mheshimiwa Nabii Mkuu Dr. Geor Davie
wa Huduma ya Ngurumo ya Upako katika ibada ya makusanyo ya vitu na fedha kwa
ajili ya kuwasaidia wahitaji alisema kuwa taasisi za dini hazina budi kujikita
katika kuwasaidia wahitaji na wasiojiweza ili kuwa na taifa imara na endelevu .
"ni
wajibu wa taasisi za kidini ,makampuni mbalimbali , hata watu binafsi
ambao wanauwezo kuweza kusaidia watu hawa wenye mahitaji na walae wasio
jiweza ili nao wajisikie vyema na kuona nao ni sehemu ya watu kama
wengine "alisema Geor Davie
Huduma hiyo
inautaratibu endelevu wa kila mwaka wa kupeleka mahitaji kwa wato wasiojiweza
pamoja na kuwawezesha kiuchumi kaya zilizoathiriwa na umasikini kwa kiasi
kikubwa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia