Diwani wa viti maalumu
Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice
|
Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice aliyevaa kitenge akiwa na baadhi ya wananchi wa wilaya ya karatu leo katika kito cha polisi mjini kati Jijini Arusha. |
Baadhi ya wananchi kutoka wilaya ya karatu wakiwa nje
ya kituo cha polisi mjini kati
Vero
Ignatus,Arusha
Sakata la
viongozi wa Chadema na wananchi wa vijijini nne wilayani Karatu Mkoani Arusha
kukamatwa na polisi kwa kosa la kuchoma mashine ya kuvutia maji
ni kufuatia haa za
baadhi ya watu kukaidi amri ya Waziri Mkuu aliyetaka mashine hizo zote
kuondolewa katika chanzo cha maji kilichokuwa na mgogoro wa muda
mrefu.
Waziri Mkuu,Kassimu Majaliwa Mnamo
desemba 5 mwaka huu,alimwagiza Mkuu wa wilaya ya
Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha
kabla ya saa 12 jioni nay eye kumaliza kikao na wananchi awe ameziondoa mashine
hizo zilizowekwa katika chanzo cha maji.
Mbali ya
hilo Waziri Mkuu aliagiza chanzo hicho
cha maji kutunzwa na mashine zote ziwe umbali wa mita 500 na mto utunzwe kwa
mita 60 tofauti na hapo hatua kali zichukuliwe.
Kufuatia
agizo hilo vifaa hivyo na vingine viliondolewa vyote kwa kusimamiwa na Mkuu wa
wilaya Karatu mwenyewe na jeshi la polisi wilaya ya
Karatu.
Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice
akizunzgumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa baada ya agizo
hilo kutekelezwa walirudi katika vikao vya jumuiya
ya uongozi wa vijiji saba vya kata mbili za Mang’ola na Qaedenti kwa
ajili ya kufanya
maazimio ya agizo la Waziri Mkuu.
Amesema
vijiji vyote viliafiki agizo hilo na kuahidi kutunza chanzo hicho cha maji
umbali wa wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho na mita 60 kutoka
kwenye mto.
Patrice ameendelea
kueleza kuwa maazimio hayo yalikubaliwa na viongozi na wananchi wa vijiji vyote
kwani kiliagizwa na Waziri Mkuu ni msisitizo kwani katika vikao vya nyuma vya
vijiji hivyo hayo yote yalikubaliwa katika vikao.
Alisema cha
kushangaza baadhi ya viongozi na madiwani kukamatwa kwani ndio waliokuwa mstari
wa mbele kuhakikisha wananchi wanatii amri ya Waziri
Mkuu.
Diwani huyo
alisema kuwa aliambiwa kuwa baadhi ya wananchi wamerudisha mashine na vifaa
vingine katika chanzo hicho cha maji na kufikia hatua ya wananchi
wengine kukasirishwa
na kitendio hicho cha kudharau mamlaka za juu
zilizoagiza.
‘’Baadhi ya
watu waliokamatwa hawahusiki kabisa na uchomwaji wa mashine hizo kwani polisi
imeamua kukamata hovyo hovyo ila mie ninachojuwa desemba 26 na 27 mwaka huu
baadhi ya wananchi walialikwa kufanya usafi katika chanzo hicho na kwa kuw
amaji yalikuwa yakipungua siku hadi siku’’alisema diwani
huyo
Mkazi
mwingine wa Kata ya Mang’ola aliyeomba kutotajwa jina lake alisema kuwa mgogoro
huo ni wa muda mrefu sana kutoka mwaka 2007 na kijiji cha Qaedenti ndio chanzo
mgogoro huo kwani wamekuwa waghumu kutii maagizo ya viongozi wa juu wa serikali
pindi wanapotakiwa kukaa umbali wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho cha
maji.
‘’wamekuwa
wakileta vurugu kila mara kwa sababu ya madai kuwa chanzo hicho ni chao lakini
sio kweli kwani chanzo hicho hutoa huduma ya maji kwa vijiji saba bila ya kuwa
na ubaguzi wowote’’alisema mwananchi huyo
Alisema
kuchomwa kwa mashine ni kutokana na wananchi kupatwa na hasira na jazba za
baadhi ya wananchi kurudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha
maji na kudharau agizo la Waziri Mkuu.
Wakati huo
huo Mbunge wa Jimbo la Karatu ,Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Karatu ,Jubillet Manyenyo wameachiwa kwa dhamana na wametakiwa
kuripoti kituo kikuu cha polisi Arusha januari 4
mwakani.
Wengine
waliokamatwa na bado wanahojiwa na polisi Arusha ni pamoja na diwani wa kata ya
Baray ,Thomas Darabe na diwani wa kata ya Mang’ola Lazaro Emmanuel
.
Kamata
kamata hiyo imewakumba wananchi wengine ambao ni pamoja na Godwin Mussa,Safari
Awak,George Pius,Baridi John,Bartazar Lohay,Jafari Thiophil,Vicent
Airo ,sebastian
Mosses na Daniel Ninida.
Wengine waliokamatwa
na polisi ambao ni ndugu ni pamoja na ndugu wawili ambao ni pamoja na Charles
Lameck na Chrisopher Lameck .
Habari
kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa baada ya kuchukuliwa maelezo kwa
watuhumiwa hao 15 majalada yanapelekwa katika ofisi ya Mwansheria wa serikali
kwa ajili ya kufungua kesi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia