Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa KamatiKuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017 ambapo amewataka watanzania wote bila kujali itikadi zao kufanya kazi kwa bidii.
Mh Lowassa ameshiriki ibada hiyo akiambatana na familia yake pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali Mkoani Arusha na Jimbo la Monduli wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mh Isack Joseph , Wakili John Mallya na viongozi wengine. |