Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka pamoja na Vijana na Viongozi
mbali mbali wa Chama Wakibeba Mwili wa Marehemu Ally Seleman aliyekuwa
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ludewa
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM)
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akisain kitabu cha wageni alipowasili katika
ofisi za CCM Wilayan Masasi
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka ,akimfariji Mzee Suleiman
Nasr,Baba Mzazi wa aliyekuwa katibu wa Umoja Wa Vijana wa CCM Wilaya ya
Ludewa Mkoa wa Njombe,Ali Nasri aliyefariki juzi na kuzikwa jana Masasi
Mkoa wa Mtwara.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa tatu kushoto Mwenye suti
Nyeusi akiwa katika kisomo cha pamoja na wanazuon mbalimbali Wilayan
Masasi Mkoa wa Mtwara
Shekh
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Al Hajj Mohammed Said Mshangani akitoa Mawaidha
msibani kwa Viongozi mbali mbali na wananchi Wilayani Masasi.
Kaimu
Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa Tano kushoto akiwa pamoja na
viongozi wa Dini ya kiislamu na Wananchi mbalimbali Wilayani masasi
wakisoma dua Mara baada ya Kuhifadhi mwili wa Marehemu Ally Nasri
aliyekuwa katibu wa UVCCM wilaya ya Ludewa katika makaburi ya Masasi.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM)
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) jana aliwaongoza viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi na jumuiya zake, wanachama na wananchi mbali mbali wa Wilaya
ya Masasi Mkoa wa Mtwara katika mazishi ya Katibu wa UVCCM wilaya Ludewa
Mkoa wa Njombe Ali Suleiman Nasir aliyezikwa kijijini kwao Masasi.
Marehemu
amefariki dunia Juzi usiku nyumbani kwao Masasi baada ya kuugua kifua
na pumu kwa zaidi ya wiki mbili ambako alikwenda kwa mapumziko ya
mwisho wa mwaka.
Akizungumza
katika mazishi hayo Ndg: Kaimu Katibu Mkuu Shaka alimtaja marehemu Ali
Suleiman Nasir kama ni kijana aliyekuwa mchapakakazi, aliyejituma kwa
bidii, aliyekuwa tayari kukosolewa na kujirekebisha kila ilipobidi na
hakuwa na nongwa.
"Tumempoteza
mtendaji tuliyekuwa tukimtegemea mno katika kupigania maslahi ya Chama
Cha Mapinduzi na jumuiya yetu mahali popote, huu ni msiba mzigo
uliogusa hisia zetu na kutuachia na majonzi makubwa katika mioyo"
Alisema kaimu Katibu Mkuu Shaka
Alimuelezea
Marehemu Nasir kuwa katika maisha yake kama mtendaji alikuwa tayari na
mwepesi kwa saa na wakati wowote kutii maelekezo toka Makao Makuu
ikiwemo na kuridhia uhamisho toka mahali pamoja kwenda pengine kila
ilipobidi na kusisitiza ingawaje pengo la Nasir linaweza kuzibika kwa
vile ametii wito wa Mwenyezimungu lakini itachukua muda mwingi chama na
jumuiya kumpata mtu wa aina yake ambaye wakati wote alijali na
kuthamini, kutimiza ahadi na maelekezo kwa ujasiri na ushupavu.
"Mwenzetu
ameitwa na Mwenyezimngu ametangulia mbele ya haki, siku zake katika
maisha ya dunia zimekwisha na hakuna mwenye uwezo wa kuzuia uamuzi wa
Mwenyezimungu, marehemu alikuwa ni mtumishi wa CCM akitumikia jumuiya ya
vijana hivyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu
Abdulrahman Omari Kinana chama kinatoa pole kwenu nyote wafiwa na
kuwaomba muwe na moyo wa subra, ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu
cha msiba, maombelezo na mtambue hili si lenu peke yenu sote tumeguswa
na ndio maana tumekuja kuwakilisha, kuwafariji na kutoa mkono wa pole
kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi na jumuiya ya Vijana" Alifahamisha
Shaka*
Marehemu
Ali Suleiman Nasir alizaliwa April 4 mwaka 1977 kijijini kwao Masasi
Mkoani Mtwara nakupata elimu ya sekondari baadae chuo cha ufundi
aliteuliwa kuwa katibu wa UVCCM wilaya Tandahimba, baadae alihamishiwa
wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara, wilaya Lushoto mkoani Tanga, wilaya
ya Same mkoani kilimanjaro aidha katika maisha yake ya utumishi ndani
ya UVCCM aliwahi kuwa katibu wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora kabla ya
kupelekwa Newala mkoani Mtwara na hadi mauti yanamfika alikuwa katibu wa
vijana wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe.
Marehemu Ali Suleiman Nasir ameacha mke na watoto watatu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia